If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, November 17, 2016

KENYA: WAZEE WA AGIKUYU WASEMA MARTHA KARUA AMEKOSA MSIMAMO

Na MWANGI MUIRURI

BARAZA la Wazee wa Agikuyu limewataka wenyeji wa Kirinyaga kutomchukulia kinara wa Narc Kenya Bi Martha Karua kwa uzito katika juhudi zake za kuwania ugavana wa eneo hilo.

Bi Martha Karua
Kiongozi wa chama cha Narc-Kenya Bi Martha Karua. Picha/VALENTINE OBARA

Kupitia kwa mwenyekiti wa baraza hilo Bw Wachira Kiago wazee hao wamesema kwa sasa Bi Karua anawachezea wafuasi wa Jubilee Party mchezo wa akili kupitia kutoa matamshi yasiyowiana na nia yake.

“Huyu Bi Karua leo anasema tumuunge mkono Rais Uhuru Kenyatta 2017. Hilo halina mjadala kwa kuwa hakuna geni hapo. Huo ndio msimamo wetu wa dhati. Kesho utamsikia akisema sio lazima rais Kenyatta aungwe mkono. Cha kuchukiza zaidi anasema yeye mwenyewe sio lazima amuunge mkono rais Kenyatta 2017,” akasema Bw Kiago akiwa mjini Murang'a mnamo Alhamisi.

Akasema: “Ukiangalia matamshi hayo kwa undani yanakuonyesha nini? Bi Karua hayuko kwa nyama na hayuko kwa ngozi. Ananing’inia tu angani akituchezea sarakasi zile za enzi za utoto za miujiza bandia ya kubadilisha maji taka kuwa soda.”

Bw Kiago amesema kuwa Bi Karua anawachukulia watu wa Kirinyaga kama majuha ambao hawawezi wakang’amua ukweli wa mambo kumhusu na pia nia yake kuu ya kisiasa.

“Huyu Bi Karua analenga tu maslahi yake binafsi. Akiwa Kirinyaga kuomba kura anawaambia wenyeji wamuunge mkono Rais Kenyatta. Akirejea alikotoka ndani ya ushirika wa Cord, anawaambia wasimuunge mkono Rais Kenyatta,” akasema.

Kutazama runinga

Amesema kuwa baraza hilo pia limeng’amua ukweli mwingine kumhusu Bi Karua ambapo “anawadharau wenyeji wa Kirinyaga kiasi kwamba hawachukulii kama walio na uwezo wa kutazama runinga.”


Akasema: “Mahojiano yake na kituo cha Citizen TV ya Jumatano ambapo alisema haungi mkono Rais Kenyatta yanamwanika Bi Karua kama asiye na ung'amuzi kuwa watu wa Kirinyaga hufuatilia vipindi vya runinga za kitaifa. Alifikiria atawapata tu Kirinyaga mashinani wakiendelea na ujuha wao na kisha awaambie wamuunge mkono Rais Kenyatta. Huyu mtu sio moto na sio baridi. 

Hana nia njema na nyumba yetu na anatusaliti kimatamshi.

Amemtaka Bi Karua kutimiza matakwa ya dharura kabla hata ya kujihusisha na siasa za Mlima Kenya: ‘Kwanza avunje chama chake cha Narc Kenya, azindue harakati za kumfanyia kampeni Rais kote nchini aliko na wafuasi wa jaribio lake la urais 2013 na hatimaye aweke matangazo angalau matatu katika magazeti na redio akitangaza yeye yuko Jubilee Party.”

Akasema: “Vinginevyo, Bi Karua hadi sasa ni mfuasi wa Cord ambaye akichaguliwa gavana wa Kirinyaga atatumia nguvu ya afisi hiyo kutuchuuza kwa mrengo ambao hatuufuati kamwe.”

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako