If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, November 9, 2016

KUMBE TRUMP NA CLINTON WALIKUWA MARAFIKI WA DHATI KABLA YA KAMPENI

Na LEONARD ONYANGO

Bi Clinton pamoja na mumewe Rais Mstaafu Bill Clinton walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria harusi ya Bw Trump alipokuwa akifunga ndoa na mkewe wa tatu, Melania Knauss, mnamo 2005.

Trump Clinton
Rais wa Amerika mteule Donald Trump amsalimia Bi Hillary Clinton. Picha/ HISANI

Bi Melania ambaye sasa atavikwa hadhi ya 'Mkewe Rais’ alikuwa mke wa tatu kufunga ndoa na Rais Mteule wa Amerika.


Mke wa kwanza wa Trump alikuwa mwanamitindo Ivana Zelnickova ambaye walifunga naye ndoa mnamo 1977 na kupata watoto watano pamoja kabla ya kutalikiana 1992.

Mwaka mmoja uliofuatia Trump alifunga ndoa na muigizaji Marla Maples ambaye walizaa naye watoto wawili kabla ya kutalikiana mnamo 1999. Bw Trump alimlipa Maples kitita cha Sh200 milioni walipotalakiana.

Rais Mteule alizaliwa mnamo Juni 14, 1946 mjini Queens, New York na alikuwa mtoto wa nne kati ya watoto watano Mary MacLeod na Frederick Trump.

Alisomea katika shule ya msingi ya New York Military Academy. Alipokuwa katika shule ya upili, Trump alikuwa mwanariadha na kiongozi wa wanafunzi.

Rais Mteule alisomea Uchumi kiwango cha digrii katika chuo kikuu cha Fordham ambapo alisoma kwa miaka miwili na kisha kuhamishiwa katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania ambapo alihitimu mnamo 1968.


Kulingana na jarida la Forbes, Bw Trump ana utajiri wa Sh370 bilioni (Dola 3.7 bilioni) ambao unatokana na mali ambayo amejilimbikizia kama vile majumba na biashara nyinginezo zilizoko katika majimbo mbalimbali nchini Amerika na mataifa ya kigeni.

Miongoni mwa mali zinazomilikiwa na Trump ni ndege ya kibinafsi aina ya Boeing 757 inayokadiriwa kuwa ya thamani ya Sh10 bilioni. Kulingana na jarida la Forbes, ndege ya kibinafsi ya Bw Trump ina vitanda vitatu na ina uwezo wa kubeba abiria 23. Jambo la kushangaza ni kwamba vifaa vilivyoko ndani ya ndege vimetengenezwa kwa dhahabu.

Bw Trump alianza kuelezea nia yake ya kuwania kiti cha urais mnamo 1999 lakini baadaye ndoto yake ikafifia. Alifufua ndoto hiyo mnamo 2013 kabla ya kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha urais kupitia chama cha Republican.

Hata hivyo, Bw Trump amekuwa akikabiliwa na sakata si haba. Miongoni mwa sakata zilizomkabili Bw Trump ni ukwepaji wa kulipa ushuru na kuwadhalilisha wanawake.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako