If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, November 16, 2016

Mawakili wa Lema waitisha faili Mahakama Kuu

NA VERONICA MHETA, ARUSHA

MAWAKILI wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wameitisha faili la kesi namba 440/441 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa madai kuwa kuna makosa ya kisheria yaliyofanywa awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa lengo la kumnyima dhamana mbunge huyo.

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha
Mawakili hao Shark Mfinanga, Peter Kibatala na John Mallya wameitisha faili hilo Mahakama Kuu na kupangwa kwa Jaji Moshi ambaye ndiye atakayesikiliza kesi hiyo na kutoa uamuzi kama uamuzi wa awali katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ulikuwa sahihi au la.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya viunga vya mahakama hiyo, wakili Mfinanga alisema wameamua kuitisha faili hilo Mahakama Kuu kwa ajili ya kujua ni kwanini Lema amekosa dhamana ambayo awali Hakimu Desdery Kamugisha alisema ipo wazi.

Alisema maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo kwa njia ya barua na yamepokewa kwa Msajili wa Mahakama hiyo Kanda ya Arusha na yamepitishwa kisha kupangwa kwa Jaji Sekela Moshi kwa ajili ya kusikilizwa.

Alisema sababu ya kuitwa kwa faili la kesi hizo mbili ni kwamba hawakuridhishwa na hatua ya Hakimu Kamugisha kumnyima dhamana Lema huku akijua kuwa alifanya kosa kwa sababu mawakili wa serikali akiwemo Paul Kadushi walisema wameonesha nia ya kukata rufaa.

Awali katika hoja za mawakili wa serikali wakiongozwa na Mwanasheria Mwandamizi Kadushi, walipinga Lema kupewa dhamana kwa madai amefanya kosa akiwa amepewa dhamana na mahakama hiyo. Pia walidai iwapo Lema atapewa dhamana kuna hatari ya usalama wa maisha yake.


Akitupilia mbalimbali hoja hizo, Hakimu Kamugisha alisema mahakama haitoi dhamana kama hisani bali ni haki ya msingi ya mtuhumiwa kama ilivyoainishwa katika Katiba ya nchi na sheria mbalimbali. Alisema iwapo mtuhumiwa ananyimwa dhamana, sheria inatakiwa kutamka bayana.

“Sheria inakataza kufinyafinya uhuru wa mtuhumiwa kupata dhamana lakini kama inabidi kumnyima dhamana ni lazima yawepo mazingira na taratibu zilizoanishwa kisheria. Nimeshindwa kupata kifungu chochote cha sheria kinachomnyima mshtakiwa dhamana akiwa chini ya dhamana,” alisema.

Alisema katika kesi hiyo namba 440 na 441 ya mwaka huu, ambazo ziliunganishwa na kuwa shauri moja, mahakama hiyo haikutoa masharti yo yote kwa mshtakiwa (Lema) asipewa dhamana iwapo atakiuka dhamana.

Kuhusu usalama wa mtuhumiwa, alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuonesha namna mshtakiwa atakavyodhurika iwapo atapewa dhamana.

Aidha alisema hakuna ukubwa wa tishio la usalama wa mshtakiwa ambao polisi wameonesha kuwa watashindwa kuuzuia.

Hata hivyo, kabla Hakimu hajatoa masharti ya dhamana, Kadushi alisimama na kuwasilisha nia ya kukata rufaa kupinga utekelezaji wa uamuzi huo akitumia kifungu cha 379(1) (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kama ilivyofanyikwa marekebisho alisema wanapinga Lema kupewa dhamana hali iliyosababisha mbunge huyo kwenda mahabusu katika Gereza la Kisongo, Arusha.

Chanzo: habarileo.co.tz

No comments:

Post a Comment

Maoni yako