If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, November 7, 2016

WAMAREKANI WAJIKUNA KICHWA KUHUSU JINA ATAKALOPEWA MUMEWE HILLARY CLINTON

Na LEONARD ONYANGO na MASHIRIKA

Amerika haijakuwa na rais mwanamke na wote walikuwa wameoa wanawake isipokuwa rais wa 15 James Buchanan ambaye alikuwa kapera.

Bill Clinton
Aliyekuwa Rais wa Amerika Bill Clinton akihutubu awali. Picha/AFP

Mbali na kuwa mumewe rais, Bill Clinton pia atakuwa rais wa kwanza mstaafu kurejea tena katika ikulu ya White House.

Bill Clinton ambaye awali alikuwa gavana wa jimbo la Arkansas alichaguliwa kuwa rais wa Amerika mnamo 1992 na kisha awamu ya pili 1996.

Kwa kawaida, Waamerika huwarejelea marais wastaafu kama ‘rais’.

Lakini endapo, Bi Hillary Clinton atashinda uchaguzi wa leo, Bw Bill Clinton atakoma kurejelewa kama ‘Rais Clinton’ atakapoapishwa kutwaa hatamu za uongozi Januari 2017.

Mtaalamu wa masuala ya nidhamu, Lisa Grotts, anakiri kuwa suala hilo ni kizungumkuti kwa raia wa Amerika.

“Nchini Amerika tuna magava sita na waume zao wanaitwa ‘First Gentleman’ (Bwana wa Kwanza). Lakini hakuna mwongozo wowote kuhusiana na waume wa marais wa kike,” akasema Grott.


“Ikiwa umewahi kuwa rais, utaendelea kuwa rais hadi kifo. Hivyo nadhani kuwa Bw Clinton ataendelea kurejelewa kama rais,” akaongezea.

Allida Black, mtaalamu wa masuala ya ikulu anasema kuwa wote Bw Bill Clinton na Bi Hillary Clinton watarejelewa kama rais watakapokuwa pamoja au katika hafla tofauti.

“Hillary atarejelewa kama Rais Clinton huku mumewe Bill akirejelewa kama rais mstaafu Clinton,” akasema Black.

“Changamoto sawa na hiyo ilishuhudiwa katika familia ya Bush ambapo George H.W. Bush alikuwa rais wa 41 na mwanawe George W. Bush rais wa 43,” akasema.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako