If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, November 8, 2016

Waziri: Tengenezeni pombe yenye ladha ya gongo

NA MAULID AHMED, DODOMA

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezishauri kampuni zinazotengeneza vilevi kutengeneza pombe yenye ladha ya gongo, kwa kuwa baadhi ya wateja wanavutiwa na ladha hiyo wana wanakipenda kinywaji hicho.

Mwijage ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma na kubainisha kuwa, gongo ikitengenezwa kiwandani itafuata ubora unaotakiwa kisheria.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Gimbi Masaba (Chadema) aliyehoji mpango wa serikali wa kuanzisha na kuhalalisha viwanda vya kutengeneza pombe aina ya gongo ili kuchochea uchumi wa nchi.

“Moja ya kigezo muhimu cha kuanzisha kiwanda ni uwepo wa soko, kutokana na wananchi kupenda kinywaji hiki(gongo) nawashauri wadau wa sekta hii kuwasiliana na ofisi za Sido ambazo zinapatikana mikoa yote ili kupata muongozo juu ya uanzishaji wa viwanda bora na salama vya aina hii,” alisema Mwijage.

Amesema haiwezekani serikali kuhalalisha gongo, ila inaishauri sekta binafsi kuanzisha viwanda vitakavyotumia malighafi zinazotengeneza kinywaji hicho kwa lengo la kuzalisha kinywaji kinachokidhi viwango vya usalama na ubora wa chakula.

Katika swali la nyongeza, Masaba amehoji kama serikali ipo tayari kufanya utafiti kujua faida zilizo kwenye gongo.


Mwijage amesema faida zinafahamika, lakini atawaelekeza wataalamu wake waendele maeneo yenye gongo na pombe nyingine za kienyeji ili kuzifanyia utafiti na zitengenezwe kwa kufuata ubora na viwango.

Chanzo: http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/17210-waziri-tengenezeni-pombe-yenye-ladha-ya-gongo

No comments:

Post a Comment

Maoni yako