If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, February 27, 2017

HAKUNA WA KUITIKISA JUBILEE RIFT VALLEY - VIONGOZI

Na BENSON MATHEKA

Wabunge na maseneta waliozungumza katika kanisa la AIC Kericho mbele ya Naibu Rais William Ruto wakanusha kwamba upinzani umepenya katika eneo hilo lililo na wapigakura wengi.


Charles Keter
Seneta wa Kericho Charles Keter na viongozi wengine wa Rift Valley wakihutubia wanahabari nje ya majengo ya Bunge awali. Picha/MAKTABA

Viongozi hao walisema wana imani kwamba eneo hilo litapigia kura wagombeaji wa Jubilee kutoka diwani hadi rais.

Baadhi ya viongozi hao ni waziri Charles Keter ambaye ni mwandani wa Naibu rais, Gavana Paul Chepkwony, naibu wake Susan Kikwai, wabunge Joseph Limo (Kipkelion Mashariki), Jackson Rop (Kipkelion Magharibi), Benjamin Langat (Ainamoi), Leonard Sang (Bureti), Erick Keter (Belgut), Justice Kimei (Soin/Sigowet) na Hellen Chepkowny ( mwakilishi wa wanawake, Kericho) na Aaron Cheruiyot ( seneta Kericho).

Walisema habari kwamba upinzani umepenya katika eneo hilo ni propaganda tupu.

"Uaminifu wetu kwa Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake Ruto na chama cha Jubilee ni imara,” alisema Bw Keter.

Aliongeza: “ Eneo hili linamuunga kikamilifu naibu rais, chama cha Jubilee na itakuwa hivyo kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti.”


Bw Ruto aliwahakikishia Wakenya kwamba serikali itatekeleza wajibu wake ili uchaguzi mkuu ujao uwe huru na wa haki na kufanyika katika mazingira ya amani.

“Tuna jukumu kama Wakenya kuhakikisha tutakuwa na uchaguzi huru, wa kidemokrasia na wa amani,” alisema Bw Ruto.
Aliwataka wote wanaogombea viti mbali mbali kudumisha amani akisema siasa za ghasia hazina nafasi kwenye karne ya 21.Chanzo:

No comments:

Post a Comment

Maoni yako