If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, February 25, 2017

KENYA: CA YAAHIRISHA KUCHUNGUZA SIMU BANDIA

Na OMAR KIBULANGA

MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (CA) imetangaza kuwa itaahirisha utekelezaji wa mfumo wa kuchunguza simu bandia (DMS) ili kutii amri ya mahakama.

Francis Wangusi
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (CA), Francis Wangusi akiongea na wanahabari jijini Nairobi, Februari 17, 2017. PichaOMAR KIBULANGA

Hatua hiyo inajiri baada ya mfumo huo kushukiwa kuwa utatumika kuwadadisi Wakenya kupitia simu zao.

“CA itaahirisha utekelezaji mfumo huo ili kutii amri za mahakama zilizotolewa Februari 20, 2017 zilizoitaka CA isitishe kwa muda utekelezaji mradi huo hadi suala hilo litakaposikizwa na kuamuliwa,” CA ilinukuliwa kwenye tangazo lao.

Hata hivyo, CA ilijitetea vikali kuwa nia yao si kutumia DMS kudadisi simu za Wakenya.
Walifafanua kuwa wajibu wa DMS ni kugundua simu bandia, simu zilizoibwa na kukwamisha mawasiliano ya kimagendo hasa kutoka humu nchini kuelekea nchi za nje.

Walisema utendakazi wa DMS hiyo utahusisha kuboresha mawasiliano kati ya kampuni mbalimbali za huduma za simu nchini ili kuzuia simu bandia kupenya kwenye mitandao yao.

“Kampuni za huduma za simu zina mifumo yao binafsi lakini haiwasiliani na wenzao, ina maana simu zilizoibwa au kudukuliwa kutoka mtandao mmoja zinaweza kutumika tena kwenye mtandao mwingine bila pingamizi,” walisema.


DMS itajenga hifadhi maalum ambapo kutanakiliwa taarifa tatu muhimu kuhusu kila simu.

Taarifa hizo ni nambari ya kipekee ya kutambulisha simu (IMEI), kitambulisho cha kampuni inayotoa huduma kwa simu hiyo (IMSI) na nambari ya mteja anayetumia simu hiyo (MSISDN).

Kisha taarifa hizo zitatumika kumtambulisha kila mteja katika kila mtandao wa simu ili kuzuia mawasiliano kutatizwa au kudandiwa na vifaa bandia.

Kutatiza mawimbi

Vifaa bandia, walisema, hutoa miale hatari inayodhuru wateja, hutumia betri feki zinazoweza kulipuka na vilevile kutatiza mawimbi ya mawasiliano.

Pia CA iliahidi kutozifunga simu bandia ambazo tayari zinatumika na wateja na badala yake kulenga zile mpya ambazo bado hazijaingia sokoni.

“Ili kuhakikisha wateja wanaotumia simu bandia hawanyimwi huduma za mawasiliano na kulinda kampuni za huduma za simu zisipate hasara, CA haitozifunga simu bandia ambazo tayari zinatumika,” walisema.

Vilevile, waliwasihi Wakenya kabla ya kununua simu wapige nambari *#06# ambapo watatumiwa nambari ya IMEI ya simu hiyo ambayo wanapaswa kuituma kupitia arafa kwa 1555 ili kuthibitisha uhalali wa simu wanayonunua.

CA ilishtakiwa na mwanaharakati Okiya Omtata baada ya Tume ya Kutetea Haki za Kibinadamu nchini (KHRC) na Shirikisho la Kutetea Maslahi ya Wateja nchini (Cofek) kuilaumu CA kwa kuazimia kuwadadisi Wakenya kutumia DMS.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako