If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, February 26, 2017

RUTO HATARINI BAADA YA UHURU NA MOI KUINGIA MKATABA

Na CHARLES WASONGA

Wanasema mwafaka kati ya Rais na mwenyekiti wa Kanu, Bw Gideon Moi unatoa nafasi kwa chama hicho kuwasilisha kivyake wagombezi wa nyadhifa nyinginezo katika uchaguzi mkuu ujao, hali inayomjenga seneta huyo wa Baringo kisiasa, hasa katika ngome ya Ruto ya Rift Valley.

William Ruto
Naibu Rais Bw William Ruto. Picha/PAUL WAWERU

Nayo Jubilee haitawasilisha mgombeaji katika kiti cha useneta wa Baringo kinachoshikiliwa na Gideon, kwa mujibu wa mkataba huo.

Hii ina maana kuwa mwanasiasa huyo hatapata upinzani mkali katika azma yake ya kuhudumu kama seneta wa Baringo kwa muhula wa pili.

Katika mkataba huo, kadhalika, Kanu itatengewa nafasi kadhaa za uwaziri huku wafuasi wake wakiteuliwa kushikilia nyadhifa za hadhi ya juu za ubalozi na katika mashirika ya serikali, ikiwa Rais atahifadhi kiti chake.

“Mkataba uliopelekea Kanu kukubali kuunga mkono Rais Kenyatta kuchaguliwa kwa kipindi cha pili hapo Agosti 8 mwaka huu unamjenga Seneta Moi kisiasa huku ukimponda hasidi wake wa kisiasa, Naibu Rais William Ruto,” anasema Profesa Edward Kisiang’ani.

Anapinga dhana kuwa uamuzi wa Kanu kumuunga mkono Rais Kenyatta ulichochewa na nia ya kufanikisha ushindi wake dhidi ya mgombeaji wa muungano wa upinzani (NASA).

“Kimsingi, hatua iliyochukuliwa na Kanu inahusu siasa za urithi wa Rais Kenyatta mwaka wa 2022 ikizingatiwa kuwa Bw Gideon ametangaza nia ya kuwania urais mwaka huo.


Hii ni kwa sababu Bw Ruto anaonekana kama mgeni katika 'kasri la mfalme’,” anaongeza mchanganuzi huyo wa masualaa ya kisiasa.

Profesa Kisiang’ani anasema hiyo ndiyo maana Rais Kenyatta amekuwa akimtembelea Mzee Moi bila kuandamana na Bw Ruto.

Kwa mfano, hivi majuzi alimzuru rais huyo wa zamani nyumbani kwake mtaani Kibera, Nairobi akiandanama na Gideon na Seneta wa Pokot Magharibi Profesa John Lonyangapuo.

Na kulingana na Profesa Herman Manyora, Rais kukumbatia Kanu ni pigo kwa naibu rais hasa ikizingatiwa Seneta Gideon na Bw Ruto wanashiriki vita vya ubabe wa kisiasa katika eneo la Rift Valley.

“Kwa hivyo, Rais Kenyatta atahitajika kucheza karata zake za kisiasa vizuri ili Ruto na wafuasi wake wasione kana kwamba wanatengwa na Rais.

Hii ni kwa sababu anahitaji kura zao katika jitihada zake za kurejea Ikulu katika awamu ya pili,” anaonya msomi huyo ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Lakini seneta mteule Paul Njoroge anatofautiana na wasomi hao wawili, akisema hatua ya Kanu ilitokana na haja na Mzee Moi kulinda mali yake.

“Kanu ni mali ya Mzee Moi. Anaitaka iunge mkono Rais Kenyatta kwa sababu anahisi salama chini ya Rais wala sio wanasiasa wa muungano wa NASA,” anasema mwanasiasa huyo ambaye majuzi aligura chama cha Jubilee na kujiunga na Kanu.

Rais Kenyatta anafahamu fika kwamba kwa misingi ya ushawishi, ndani na nje ya Rift Valley, Naibu Rais, Bw Ruto anamzidi Seneta wa Baringo. Kwa hivyo, anafahamu atapoteza nafasi yake ya kushinda katika uchaguzi mkuu ujao endapo wafuasi wa naibu wake watahisi kusalitiwa.

Lakini kwa upande mwingine, Rais ameonakana kujipata katika njia-panda maana hangependa kwenda kinyume na matakwa ya Mzee Moi ambaye alimlea kisiasa tangu mwaka wa 1997.

Rais huyo wa zamani haelewani na Ruto, kisaisa, kwa sababu aliwahi kukaidi maagizo yake na badala yake akamuunga mkono Raila Odinga (2007).

Tayari wandani wa Ruto wamepuuzilia mbali mkataba kati ya Rais Kenyatta na Kanu, wakidai unahusu “watu ambao wanaogopa ushindani”.

Woga

“Huo ni mkataba wa watu ambao tayari wameingiwa na woga baada ya kung’amua wamepoteza ushawishi wa kisiasa na hivyo watashindwa.

Tuna mwaniaji wa kiti cha useneta Baringo na tunaamini ataibuka mshindi,” Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen alinukuliwa akisema.

Kauli yake inaungwa mkono na kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale.

Bw Murkomen alikuwa akirejelea Mkurugenzi wa Bodi ya Kudhibiti Mchezo wa Kamari (BCLB), Bw Simon Chelugui ambaye ameidhinishwa na Bw Ruto kuwania kiti cha useneta wa Baringo kwa tiketi ya chama cha Jubilee (JP).

Awali, Bw Chelugui alikuwa akimezea mate kiti cha ugavana wa Baringo lakini naibu rais akamshauri kubadili nia.

Murkomen na Duale ni wandani wakuu wa Naibu Rais na ambao semi zao hufasiriwa na kuaminika kuwakilisha msimamo wa kiongozi huyo ambaye anatambuliwa kama mwanasiasa mkakamavu.

Kauli ya Murkomen ilionekana kulandama na ile iliyotolewa na msimamizi mkuu wa makao makuu ya JP, Bw Raphael Tuju aliyesema kuwa chama hicho hakitambui vyama vidogo vitakavyowasilisha wagombeaji kivyao hata kama vitamuunga Rais.

Profesa Manyora anaonya huenda makabiliano makali yakashuhudiwa kati ya wafuasi wa Kanu na Jubilee hasa katika Rift Valley wakati wa kampeni “ikiwa makubaliano kati ya Rais Kenyatta na Seneta Moi yatadumishwa.

“Taswira ya ushindani kati ya Kanu na Jubilee, iliyoshuhudiwa katika uchaguzi mdogo wa useneta wa Kericho mapema mwaka jana huenda ikarejelewa hasa katika ngome ya Naibu Rais ya Rift Valley.

Hii ni kwa sababu Bw Ruto na Seneta Moi watakuwa wakiwafanyia kampeni wagombeaji wa vyama vyao katika majukwaa tofauti huku wakijiandaa kwa kinyang’anyiro cha 2022,” anasema.

Hii, anasema, huenda ikaathiri kampeni za Rais Uhuru Kenyatta katika eneo hilo linaloongoza kwa idadi ya kura.

Kulingana na hesabu za kura zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi (IEBC) kwa jumla eneo hilo lina zaidi ya kura 4 milioni, ambazo Rais Kenyatta atahitaji kujihakikishia ushindi.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako