If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, March 12, 2017

ALLY BUSHIR: Anavyoinusuru Mwadui

Na IMEANDIKWA NA ALEXANDER SANGA

KOCHA Ally Bushir ni mmoja wa makocha wakubwa nchini aliyezaliwa Juni 28, 1965 Kikwajuni Zanzibar.

Ally Bushir
Ally Bushir

Kocha huyo ambaye mashabiki wake wengi hupenda kumwita kwa jina la utani Bush ikiwa ni kifupi cha Bushiri, alianza kujizolea umaarufu tangu akiwa anacheza mpira nafasi ya mlinda mlango.

Katika mahojiano maalumu na gazeti hili Bush anasema soka lipo kwenye damu yake kwa muda mrefu tangu akiwa mtoto mdogo ambapo alikuwa mchezaji mahiri Zanzibar na viunga vyake.

“Nilianza kucheza mpira rasmi nikiwa na umri wa miaka sita katika timu ya Nyuki FC ya Zanzibar mwanzoni mwa miaka ya sabini. Ligi Kuu ya Zanzibar nilianza kucheza na timu ya Kikwajuni FC mwaka 1978-1980,’’ anasema Bushir. Baada ya kudakia timu ya kikwajuni FC Bushir alijiunga na timu ya soka ya Small Simba ambayo nayo ilikuwa Ligi Kuu ya Zanzibar.

Bushir alicheza timu hiyo kwa miaka mitano tu na baada ya hapo akatimkia timu ya Malindi FC(1988-1996). Kocha huyo alistaafu akiwa na timu ya Mlandege FC ambapo alicheza klabu hiyo kwa miaka miwili tu kisha akastaafu 1999.

“Niliamua kustaafu maana umri ulikua umeenda kiasi na lakini pia vijana ambao niliwafundisha mimi mwenyewe walikua tayari wamekua na wanafanya vizuri katika Ligi Kuu, hivyo nilione niwape nafasi ili wacheze kwa kujinafasi, kwani ingekuwa shida kwao kuona mwalimu wao tangu utotoni mwao nipo golini na kuna wakati walikuwa wakikataa kucheza na timu ninayochezea mimi, lakini pia pamoja na hayo nilitaka kustaafu kwa hesima nikiwa bado kwenye uwezo mzuri,” anasema.

Bushiri mwenye leseni B ya ukocha ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) alidumu katika timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 1982-1985 na pia aliidakia timu ya taifa, Taifa Stars kati ya mwaka 1983 mpaka 1994.


“Wakati bado nacheza soka la ushindani nakumbuka nilishawahi kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar mara nne mfululizo kuanzia 1983 mpaka 1987. Nilichukua tena ubingwa wa ligi nikiwa na Malindi (Zanzibar) kuanzia 1989 mpaka 1996,” anasema.

Kwa mujibu wa kocha huyo, akiwa na timu ya Malindi alitwaa ubingwa wa ligi ya Muungano mwaka 1992 huku akitwaa tuzo ya kipa bora wa wa Ligi Kuu ya Zanzibar mwaka 1984 mpaka 1987 akiwa na klabu ya Small Simba na kutwaa tena tuzo hiyo mwaka 1988-1996 akiwa na Malindi.

“Nimecheza michuano mbali mbali ya Chalenji nikiwa na timu ya Taifa ya Zanzibar pia michuano mingine ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) nikiwa na timu za Small Simba na Malindi FC,’’ Bushir alisema. Tuzo ya kipa bora haikumkauka alipokuwa akicheza, kwani alitwaa tena tuzo hiyo kwenye michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) mwaka 1992.

Katika safari yake ya ukocha, Bushir alizipandisha Ligi Kuu timu za Stone Town na ile ya Baghdad FC kutoka daraja la pili kwenda la kwanza. Timu zote hizo ni za Zanzibar. Bushiri aliwahi kuwa kocha wa KMKM Zanzibar na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu misimu miwili mfululizo 2012/2013 na 2013/2014.

Kocha huyo mchangamfu pia aliwahi kuzifundisha timu za FC Cologne, Baghdad FC (Ligi daraja la pili, Zanzibar), Polisi FC, Stone Town FC, Small Simba FC, Malindi FC, KMKM FC zote zinashiriki Ligi Kuu ya Zanzibar.

Wakati rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete alipoamuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuajiri kocha wa kigeni, aliletwa Mbrazili Marcio Maximo mwaka 2008 na Bushiri akateuliwa kuwa msaidizi wake, anazungumziaje nafasi hiyo? Bushiri anasema Maximo alimnyanyua kutoka hatua aliyokuwa nayo wakati huo na kumpandisha juu zaidi.

“Na ukweli kiutendaji wa kazi kwa weledi ni yeye ndo aliyenifungua akili yangu zaidi kwa vile alivyokuwa wakati mwingine akinipa kazi za kuandaa programu za mazoezi na pia katika mazoezi nilikuwa nafanya uchambuzi wa kazi ambazo alinitaka nifanye na nakusanya vitu muhimu nampatia na yeye alikuwa akinitaka mimi ndio nizifanyie kazi kimaandishi na nimkabidhi,” anasema.

“Hivyo kifupi ni kuwa alinipa uzoefu mkubwa katika kazi hii ya ukocha. Na kuhusu utendaji wake yeye katika kazi kwa kweli Marcio alikuwa ni mtu makini na kazi na alikuwa akinitaka kila wakati ninapokuwa uwanjani kuelekeza akili kwenye kazi na si vinginevyo pia alikuwa hana mbadala katika suala la nidhamu, akisema bila ya nidhamu hakuna kazi, ni kifupi kwa niliyojifunza kwa Marcio,” anasema.

Kwa sasa kocha huyo ameingia kwenye soka ya Bara, akifundisha timu ya Mwadui ya Shinyanga tangu ulipoanza mzunguko wa pili mwishoni mwa mwaka jana. Awali Mwadui ilikuwa chini ya Jamhuri Kihwelo, Julio aliyebwaga manyanga mwishoni mwa mzunguko wa kwanza akidai waamuzi wanaionea timu yake.

Julio aliondoka akiiacha Mwadui ipo kwenye hali mbaya, lakini sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 31 na ikipambana zaidi inaweza kubaki Ligi Kuu. Akizungumzia timu hiyo, Bushiri anasema aliikuta kwenye hali mbaya na kazi kubwa anayofanya ni kuhakikisha inabaki Ligi Kuu, jambo analoamini linawezekana.

Hata hivyo, hajajua hatima yake maana anasema walikubaliana na viongozi asaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu lakini mpaka sasa hajapewa mkataba wenyewe.

“Hivyo hatima yangu nitaijua tukimaliza ligi kama nitabaki au nitakwenda kwingine kufanya kazi maana sitakuwa na cha kunifunga kwa vile sina mkataba nitakuwa huru kubaki au kwenda popote ninapopataka,” anasema.

Bushiri tayari amepata uzoefu wa kufundisha kwenye ligi ya Zanzibar na Bara, anasema kuna tofauti kubwa kwenye ligi hizo.

“Tofauti ni kubwa sana, kwanza ligi ya bara ni ligi yenye ushindani sana na hamasa iko juu kwa mashabiki na zaidi wachezaji wanapopambana kiwanjani na pia ni ngumu kwa vile timu zinasafiri umbali mrefu kucheza mechi tofauti na Zanzibar ligi imekuwa nyepesi haina ushindani na hamasa kama ilivyo huku,” anasema.

Chanzo: habarileo.co.tz

No comments:

Post a Comment

Maoni yako