If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, March 31, 2017

BAJETI: FURAHA KWA WAKENYA, UGALI SASA NAFUU

Na VALENTINE OBARA na CHARLES WASONGA

NI furaha tele kwa Wakenya sasa baada ya Waziri wa Fedha Henry Rotich kupendekeza ushuru unaotozwa mahindi na ngano upunguzwe. Wakenya sasa wataweza kupika mlo wao wa ugali bila kidhibiti cha bei.

Henry Rotich
Waziri wa Hazina ya Kitaifa, Henry Rotich, Machi 30, 2017 nje ya jengo la Hazina kabla ya kuenda bungeni kusoma bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/2018. Picha/SALATON NJAU

Akisoma bajeti ya mwaka wa 2017/2018 katika Bunge la Taifa Alhamisi, Bw Rotich alisema hatua hiyo imelenga kuwapunguzia wananchi gharama ya maisha ambayo imekuwa ikipanda kwa kasi.

Waziri amechukua hatua hiyo wakati ambapo ripoti zinaonyesha idadi kubwa ya wananchi wa kawaida wamepunguza kula ugali na badala yake kula chapati zaidi kutokana na bei ya juu ya unga wa mahindi isiyopungua Sh140 kwa pakiti ya kilo mbili.

“Ninatarajia watengezaji wa bidhaa za unga wa mahindi na ngano watapunguza bei ya bidhaa hizo la sivyo hatua hii itabatilishwa,” akasema Bw Rotich.

Katika hali hiyo hiyo ya kuwezesha Wakenya wengi kufurahia mlo wao wa ugali wanaopenda zaidi, waziri alitangaza kuondolewa ushuru wa kuagiza mahindi kutoka mataifa ya kigeni.

Kunyimwa faida

Hata hivyo, hatua hiyo haikufurahisha wabunge kutoka maeneo ambako kilimo cha mahindi ni tegemeo kubwa zaidi la mapato yao, kwani inamaanisha kuna uwezekano mkubwa bei ya mahindi itashuka na kuwanyima faida kubwa wakulima.


Bei ya samaki wanaovuliwa baharini pia inatarajiwa kushuka baada ya waziri kupendekeza ushuru uondolewe kwa vifaa vya kupakia samaki na vifaa vingine vinavyotumiwa katika shughuli zote za uvuvi huo.

Bw Rotich anapendekeza malipo ya bandarini kwa vyombo vya uvuvi baharini yapunguzwe kwa asilimia 50.

Wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 70 watakuwa wakipewa pesa za matumizi kila mwezi na pia kulipiwa pesa za Hazina ya Kitaifa Matibabu (NHIF).

Ujenzi, kilimo na utalii

Mbali na wananchi wa kawaida, sekta kadhaa zinatarajiwa kunufaika kutokana na bajeti hiyo kwani zimeondolewa ushuru tofauti tofauti.

Katika sekta ya ujenzi, Bw Rotich alipendekeza ushuru uondolewe kwa mafuta yanayotumiwa kutengeza rangi ya nyumba.

Sekta ya kilimo itanufaika kwa kuondolewa ushuru wa bidhaa za kutengeneza dawa za kuangamiza au kuzuia wadudu wa mimea.

Ili kuimarisha sekta ya utalii, bajeti hiyo imependekeza ushuru uondolewe kwa magari ya kusafirisha watalii yanayotengezwa humu nchini.

“Wawekezaji katika utalii watahimizwa kununua magari ya kusafirisha watalii kutoka kwa viwanda vya humu nchini,” akasema Bw Rotich.

Afya

Sekta ya afya, ambayo imekumbwa na changamoto nyingi katika utawala wa Serikali ya Jubilee, pia haikusahaulika. Bajeti imependekeza ushuru uondolewe kwa vifaa vya matibabu vinavyotumiwa katika hospitali za matibabu maalumu.

Kwa walioajiriwa, serikali imependekeza mshahara wa chini zaidi unaoweza kutozwa ushuru uwe Sh13,486 kwa mwezi, tofauti na Sh11,135 ilivyokuwa awali. “Hii itaongezea idadi kubwa ya wenye mishahara ya chini kiwango cha pesa wanachobaki nacho,” akasema.

Bajeti hiyo ya mwisho ya Serikali ya Jubilee kabla uchaguzi wa Agosti itajadiliwa na kupitishwa na Bunge kabla ya kutekelezwa.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako