If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, March 10, 2017

Hawaii yaenda kotini kupinga sheria ya kibaguzi ya Trump

Jimbo la Hawaii nchini Marekani limepeleka faili la kesi mahakamani kupinga sheria mpya ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo iliyo dhidi ya Waislamu.

Jaji Derrick Watson wa Mahakama ya Federali mjini Honolulu, jimbo la Hawaii anatazamiwa kusikiliza kesi hiyo mnamo Machi 15. Sheria hiyo mpya ya kibaguzi ya Trump inakabiliwa na wimbi la lalama na ukosoaji kutoka kila upande, ndani na nje ya nchi.

Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia ambaye pia ana uraia wa Marekani juzi Jumanne wakati wa safari ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwamba alikosoa amri hiyo ya Trump na kutoa wito wa kufutwa kabisa, akisisitiza kuwa, Wasomali wamesaidia uchumi na jamii ya nchi hiyo kwa msingi huo idadi ndogo ya wale wanaoweza kusababisha matatizo wanapaswa kushughulikia kivyao.

Trump akisaini agizo jipya la kibaguzi dhidi ya nchi za Kiislamu

Kadhalika asasi za kutetea haki za binadamu kama Human Rights Watch, United Farm Workers of America na The New York Immigration Coalition pamoja na mashirika ya kidini likiwemo la Interfaith Alliance, yamekosoa vikali sheria hiyo na kuitaja kuwa ya kibaguzi na inayokiuka katiba.

Katika sheria hiyo mpya, Trump ameiondoa Iraq katika orodha ya nchi saba za Kiislamu ambazo raia na wakimbizi wake hawataruhusiwa kuingia nchini Marekani katika muda wa siku 90 zijazo. Nchi zilizoathiriwa na sheria hiyo ya kibaguzi ya Trump ni Sudan, Somalia, Syria, Iran, Libya na Yemen.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako