If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, March 9, 2017

Japan: Ni lazima tujiandae kukabiliana na mashambulizi tarajiwa ya Korea Kaskazini

Waziri wa zamani wa Ulinzi Japan ametaka kuimarishwa uwezo wa kijeshi kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi tarajiwa ya Korea Kaskazini.

Itsunori Onodera, Waziri wa Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Japan ambaye kwa sasa ni mkuu wa Baraza la chama tawala nchini humo, amesema kuwa, harakati zozote za kijeshi za Korea Kaskazini dhidi ya Japan, zitakabiliwa na jibu mbadala. Matamshi hayo yamekuja kufuatia hatua ya hivi karibuni ya Pyongyang ya kuvurumisha makombora manne katika maji ya Japan.

Itsunori Onodera, Waziri wa Waziri wa zamani wa Ulinzi Japan

Duru za habari zinaeleza kuwa, viongozi wa Tokyo wamekusudia kuchukua hatua kali katika sera za kiulinzi katika kukabiliana na hatari dhidi yake. Moja ya mambo yanayowatia wasi wasi mkubwa viongozi wa Japan ni kwamba, mwezi uliopita, Korea Kaskazini iliboresha zaidi mfumo wa mafuta ya kuchochea makombora yake kwa kuufanya kuwa mgando. Kabla ya hapo Pyongyang ilikuwa ikitumia mafuta laini katika shughuli za ufyatuaji makombora.

Sehemu ya makombora ya jeshi la Korea Kaskazini

Hatua ya hivi karibuni ya Korea Kaskazini kufyatua makombora yake manne katika maji ya Japan, iliifanya Washington kutuma nchini Korea Kusini mfumo wake wa ulinzi wa makombora wa THAAD, ambao umekuwa ukilalamikiwa na nchi za China, Russia na Korea Kaskazini. Taarifa iliyotolewa na Pyongyang ilisema kuwa, jaribio lake hilo la makombora ni maandalizi kwa ajili ya kuzishambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Japan.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako