If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, March 13, 2017

JOHO ALIVYOHANGAISHWA NA MAAFISA WA GSU

Na LEONARD ONYANGO

GAVANA wa Mombasa Hassan Joho na mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba Jumatatu asubuhi ‘walifungiwa’ ndani ya afisi na maafisa wa GSU baada ya kuzuiliwa kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Feri ya Mtongwe iliyohudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Ali Hassan Joho
Gavana wa Mombasa (kati) Ali Hassan Joho alipozuiliwa na maafisa wa GSU Machi 13, 2016 katika daraja la Nyali, Mombasa. Picha/ HISANI

Wawili hao walikamatwa na maafisa wa GSU walipokuwa wameabiri pikipiki, kuepuka msongamano wa magari barabarani, wakielekea katika hafla hiyo.

Akihutubia wanahabari afini kwake, Gavana Joho alisema polisi waliagizwa kutowaruhusu (Joho na Bedzimba) kutotoka nje ya afisi hadi pale Rais Kenyatta atakapoondoka jijini Mombasa.

Bw Joho alisema maafisa wa GSU walimzingira nyumbani kwake katika eneo la Nyali, alfajiri, kwa lengo la kumzuilia kuhudhuria hafla ya Rais Kenyatta.

“Nilifanikiwa kutoroka bila maafisa wa GSU kuniona na kuelekea katika hafla hiyo. Mimi nikiwa kiongozi nilihitaji kuwepo ili kuwakilisha watu wangu wa Mombasa,” akasema Bw Joho.


"Nilikuwa na nia njema lakini sasa nimezuiliwa kuhudhuria hafla hiyo na sasa niko chini ya ulinzi mkali afisini,” akasema Bw Joho ambaye ni mwendani wa karibu wa kinara wa ODM Raila Odinga.

Hayo yanajiri siku moja baada ya polisi kumnyima kibali Bw Joho cha kufanya mkutano wa kisiasa katika uwanja wa Mvita kutokana na sababu za kiusalama kwa kuwa rais Kenyatta alikuwa na mkutano sambamba katika uwanja wa Tononoka.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako