If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, March 6, 2017

JOHO ALIVYOPOKELEWA KISHUJAA BAADA YA ZIARA AMERIKA

Na LUCAS BARAZA

Bw Joho alitangaza kwamba wakazi wa Mombasa na eneo la pwani kwa jumla watakutana katika uwanja wa Tononoka Machi 27 kutangaza msimamo wao wa kisiasa.

Ali Hassan Joho
GAVANA wa Mombasa, Ali Hassan Joho awahutubia wafuasi wake mjini Mombasa baada ya kurejea nchini kutoka Amerika Machi 5, 2017.

Alisema hatishwi na madiwani kadhaa na viongozi wengine waliohama ODM na kujiunga na chama cha Wiper akiwa Amerika kwa wiki mbili akisisitiza kuwa eneo la pwani ni ngome ya ODM.

“Ni watu wachache waliohama ODM lakini wanaojiunga na chama ndio wengi,’ alisema.

Bw Joho ambaye ni mwandani wa Bw Odinga alipuuza vyama washirika wa NASA; Wiper Party na Amani National Congress pamoja na chama cha Jubilee akisema wakazi watapigia kura ODM.

Kwenye uchaguzi mkuu wa 2013, wakazi wa Pwani walipigia ODM kura kwa wingi na kikashinda asilimia 90 ya viti vyote.

Katika Kaunti ya Mombasa, chama hicho kilishinda viti 30 vya udiwani. Mwezi jana, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka aliuliza wafuasi wake kwa nini chama hicho hakikushinda hata kiti kimoja cha udiwani na akawataka kubadilisha hali kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Wiper kilipigwa jeki wiki jana, aliyekuwa waziri Chirau Ali Mwakwere alipohamia chama hicho.

Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi jana alikuwa Mombasa baada ya kutembelea Kilifi mwezi uliopita kuvumisha Nasa.

Naibu Rais William Ruto pia alitembelea Mombasa, Kilifi, Kwale na Taita Taveta kupigia debe JP.

Jumapili, Bw Joho alitangaza: “Mombasa ni ngome ya ODM na ni wagombeaji wa chama hicho ambao watashinda kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti.”


Alisema ODM kina mshindani mmoja ambaye ni chama cha Jubilee.

Uongozi mbaya

Ingawa wako Nasa, Katibu Mkuu wa Wiper Hassan Omar na mbunge wa Nyali Hezron Awiti, wamezidisha kampeni za kumshinda Bw Joho wakimlaumu kwa uongozi mbaya. Hata hivyo, wawili hao watamenyana kwanza katika mchujo wa Wiper.

Mnamo Jumamosi, Bw Omar alikataa uteuzi wa pamoja kwa Nasa Mombasa.

Hata hivyo, Bw Joho alisema jana kwamba kamati maalumu ya Nasa ndiyo itaamua mfumo wa uteuzi na wafuasi hawafai kuyumbishwa na maoni ya watu binafsi. Akiongea alipotembelea maeneo ya Changamwe, Jomvu na Frere Town, Bw Joho alisema msimamo wa Nasa ni kwamba uteuzi utakuwa huru na wa haki.

“Nasa ina kamati ya kupanga shughuli zake ukiwemo uteuzi. Mpinzani wetu ni Jubilee. Mpinzani wangu ni Jubilee na sio hao majamaa wengine,” alisema akishangiliwa na wakazi wa Mikindani.

Wafuasi wake walifika kwa wingi katika uwanja wa ndege wa Moi kumkaribisha. Shughuli zilisimama kwa muda katika uwanja huo na polisi walikuwa na wakati mgumu kuwadhibiti watu waliokuwa wakicheza ngoma.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako