If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, March 30, 2017

JOHO ATII AGIZO, AFIKA KITUO CHA POLISI

Na MOHAMED AHMED na DANIEL NYASSY

GAVANA wa Mombasa amedai kuwa polisi walikuwa wameandaa hati ya mashtaka ili wamkamate na kumfikisha mahakamani.

Hassan Joho
Gavana Hassan Joho akiwa na mawakili wake, viongozi na wafuasi katika barabara ya Ikulu karibu na makao makuu ya Polisi Pwani kuhojiwa kuhusu cheti cha kidato cha nne Machi 29, 2017. Picha/KEVIN ODIT

Joho alisema kuwa wakati alipokuwa anaandikisha taarifa yake Jumatano katika ofisi za makao makuu ya kitengo cha CID jijini Mombasa, aliona hati hiyo ikiwa imewekwa kando kwa kusudio la kumfikisha mahakamani.

“Nilipokuwa ndani kule niliona kuwa wameweka hati hiyo tayari ili wanipeleke korokoroni. Nilikuwa na mawakili wangu wakiwamo Seneta James Orengo, Gavana Amason Kingi na Mohammed Balala na wengine ambao walikuwa tayari kupambana na wao mahakamani,” akasema Bw Joho.

Alisema kuwa madai hayo ya kutengeneza cheti bandia ambayo ndiyo alikuwa ameitiwa kwenda kuandikisha taarifa kuyahusu ni porojo na mpango wa kuhakikisha hawi katika debe la uchaguzi wa Agosti 8.

“Hayo madai ni porojo tupu na uongo mwingi. Nawaambia watu wa Mombasa kuwa wanafanya haya ili wawatie uoga kuwa sitokuwa katika debe lakini nawahakikishia kuwa iwapo nitakuwa mzima nitakuwa debeni,” akasema Joho.

Joho alikuwa akizungumza na wafuasi wake nje ya ofisi zake za Treasury Square ambayo iko kilomita chache na ofisi za CID.


Hata hivyo, kuhusu madai ya iwapo kulikuwa hati ya mashtaka iliyokuwa imetayarishwa, Mkuu wa CID eneo la Pwani, Pius Macharia hakupokea simu wala kujibu jumbe alizotumiwa na Swahilihub.

Vilevile kulingana na mdokezi wetu katika taarifa yake kwa polisi, Joho alikanusha kutengeneza cheti hicho kilichoonyesha kuwa amepata alama ya C+ na kuwa hakuwa katika chuo kikuu cha Nairobi kama inavyodaiwa.

Kurahisisha maisha

Wakati huo huo, Joho alimshambulia Rais Uhuru Kenyatta na kusema kuwa angetumia nguvu hizo anazotumia kumuandama yeye azibadilishe katika kuwarahisishia Wakenya maisha

Alisema kuwa hatobadilisha msimamo wake dhidi ya “uongozi mbaya” wa serikali ya Jubilee na kuongeza kuwa Mungu ndiye mwenye nguvu zaidi.

“Mimi naogopa Mungu peke yake ambaye ndiye mwenye uwezo kushinda yoyote yule. Viongozi wa Jubilee hawawezi kuwa miungu. Naomba Mungu kuwa Wakenya watageuza nguvu hizo hizo kupeleka serikali ya Jubilee nyumbani,” akasema.

Orengo na Bw Kingi walisema kuwa watasmimama na Bw Joho katika kupigana vita hivyo ambavyo waliviita kuwa ni porojo na uongo mtupu.

Orengo alisema kuwa atafanya chochote kile kuhakikisha kuwa hakuna mtu anafanikiwa kumkaribia Bw Joho kwa ni mbaya.

“Nataka kuwambia nyinyi watu wa Mombasa musiwe na hofu kwani hii kesi tutashinda tu. Tunajua Jubilee wameingia uoga baada ya ule mkutano wa Tononoka juzi. Tunawambia wakidara Joho itakuwa wanadara Raila Odinga na nchi nzima kwa jumla,” akasema.

Kwa upande wake Joho alisema kuwa madai hayo anayoandamwa nayo yalikuwa ni kesi ya “kisiasa” na sio kesi ya kisheria.

“Jubilee wanatumia vyombo vya dola kupigana na Joho lakini tunawaambia kuwa hawatotutisha maana kila wakizidi kumuandama Joho ndiyo wanamtia makali zaidi. Hii ni kama vile ukifinyanga chungu ukiweke kwa moto kikitoka motoni humu huwa hakivunjiki tena,” akasema Kingi.

Hapo asubuhi, viongozi hao walikuwa wameandamana na wafuasi wao katika ofisi hizo ambapo walionekana wakitembea kwenda na kurudi kutoka ofisi za Bw Joho ambazo ziko umbali wa kilomita chache tu na afisi za CID.

Viongozi hao walikaa ndani humo zaidi ya saa mbili katika afisi hizo. Viongozi wengine waliokuwa wameandamana na Bw Joho walikuwa ni Dkt Agnes Zani, wabunge Abdulswamad Nassir (Mvita), Rashid Bedzimba (Kisauni), Omar Mwinyi (Changamwe), Badi Twalib (Jomvu), Suleiman Dori (Msambweni) na Mishi Mboko miongoni mwa wengine.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako