If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, March 29, 2017

KAMATAKAMATA YAIBUA VURUGU NAMANGA

Na MUSSA JUMA, ARUSHA, Tanzania

SHUGHULI katika mpaka wa Kenya na Tanzania wa Namanga uliopo wilayani Longido mkoani Arusha zilisimama Jumatatu kutokana na uamuzi wa baadhi ya raia wa Kenya wanaoishi upande wa nchi hiyo kuufunga mpaka kwa kuchoma matairi ya magari na kuandamana.

Namanga 
Barabara ya kuenda kwa ofisi za idara ya uhamiaji mjini Namanga; mpakani Kenya na Uganda palitokea maandamano Wakenya wakidai wanahangaishwa na maafisa wa Tanzania Machi 27, 2016. Picha/JOSEPH NGUNJIRI

Walifikia hatua hiyo wakipinga kamatakamata ya wahamiaji haramu wanaoishi upande wa Tanzania ambayo inafanywa na idara ya uhamiaji kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Longido.

Jumatatu Mkuu wa wilaya hiyo Daniel Chongolo akizungumza na Swahilihub alisema kitendo cha baadhi wa wananchi wa nchi jirani kufunga mpaka na kuchoma matairi barabarani hakitazuia operesheni inayoendelea ya kusaka wahamiaji haramu.

Alisema msako huo unafanyika baada ya kubainika kuna zaidi ya kaya 80 za raia kutoka Kenya zinaishi upande Tanzania bila kufuata utaratibu.

Chongolo alisema kuna raia wa nchi jirani wamekamatwa kwa kuishi nchini kinyume cha utaratibu na hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kutolewa siku saba kwa wote ambao wanaishi upande wa Tanzania kinyume na utaratibu waende ofisi za uhamiaji ili wapate vibali.

Alisema baadhi yao walikaidi lakini operesheni ilipoanza juzi imefanikisha kuwakamata.


“Tumekubaliana wale wote wanaoishi kinyume na utaratibu wafuate sheria. Pia kutoingilia uhusiano na jirani zetu za mpaka ambao unaruhusu mtu kuingia nchi nyingine kilomita 10 na kurudi na siyo kuishi,” alisema.

Alisema shimikizo linaloendelea halitakubalika kwa kuwa tayari wamefikia makubaliano ya kumaliza mgogoro kwa kuzingatia sheria.

Diwani wa Namanga, Hussein Ngoma alisema pande zote wamekubaliana kufuata sheria na ambao watakaidi hatua zitachukuliwa.
/

No comments:

Post a Comment

Maoni yako