If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, March 21, 2017

KENYA: RAIS AONYA WANAOCHOCHEA VITA VYA KIJAMII

Na SAMMY WAWERU

Rais Kenyatta amewaonya wanaoeneza vita vya kijamii katika Kaunti za Baringo na Laikipia.

Citizen Nipashe
Rais Uhuru Kenyatta ahojiwa na wanahabari wa Citizen Nipashe, Kanze Dena na Lulu Hassan Machi 20, 2017 katika Ikulu ya Nairobi. Picha/PSCU

RAIS Uhuru Kenyatta amewaonya wanaoeneza vita vya kijamii katika Kaunti za Baringo na Laikipia.

Rais Kenyatta amewaonya vikali wanaoeneza vita katika Kaunti ya Baringo na Laikipia kufuatia vita vya kijamii ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa katika kaunti hizi.

Aidha, kiongozi huyu wa taifa ameshikilia kwamba serikali haitastahimili kuona maisha ya watu yakiangamia katika kaunti hizo.

"Hatutaruhusu kuona maisha ya watu yakichukuliwa na watu wengine" akasema Rais Kenyatta akihojiwa Jumatatu na wanahabari wa Citizen Nipashe, Kanze Dena na Lulu Hassan.

Wakati huo huo Rais Kenyatta ametahadharisha wanaomiliki silaha hatari kinyume na sheria.

"Hatutakubali watu wamiliki silaha 'bandia' sharti zirejeshwe kwa serikali," alionya huku akirejelea wanaomiliki silaha hatari kinyume na sheria Kaunti za Laikipia na Baringo.


"Nilituma naibu wangu maeneo yanayoshuhudia vita hivyo kwa sababu nimejitolea kwa hali na mali kuchunga maisha ya wananchi" akasema Rais Kenyatta.

Akaongeza, "Ngoja wanaoeneza chuki na vita vya kijamii maeneo hayo wataona yatakayotokea hivi karibuni."

Haya yanajiri serikali wiki iliyopita kutuma vikosi vya wanajeshi kuendesha oparesheni katika Kaunti ya Baringo ili kuleta amani na kutwaa silaha hatari zinazomilikiwa kinyume na sheria na wahalifu wanaoeneza vita hivyo.

Vita vya kijamii vinavyoshuhudiwa Kaunti ya Laikipia na Baringo vinashukiwa kuwa na ushawishi wa kisiasa kutoka kwa baadhi ya viongozi kutoka maeneo hayo.

Jamii zinazoishi kaunti hizo zimekuwa zikizozana kwa wizi wa mifugo, ardhi na lishe ya mifugo wao na kusababisha vifo vya watu na wengine kuhama makwao wakihofia usalama wao.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako