If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, March 5, 2017

KIMYA NDANI YA JUBILEE CHAIBUA HOFU KUU

Na BENSON MATHEKA

Viongozi hao wawili hawajakuwa na mikutano mikubwa ya hadhara tangu wakamilishe kampeni ya kuwarai wakazi wa ngome zao kujisajili kwa wingi kupiga kura shughuli iliyokamilika Februari 19 mwaka huu.

Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta. Picha/DIANA NGILA

NASAinayoshirikisha vyama vinne vikuu, ODM, Wiper, Amani National Congress na Ford Kenya imekuwa ikiandaa mikutano mikubwa ya hadhara katika ngome za Jubilee ambayo imekuwa ikivutia watu wengi. Mkutano wa kwanza ulifanyika katika uwanja wa 64 mjini Eldoret Kaunti ya Uasin Gishu na nyumbani kwa Naibu Rais Ruto.

Mapema wiki hii, vinara wa NASA, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetang’ula walipeleka kampeni za kuvumisha muungano wao kaunti za Meru na Tharaka Nithi ambako waliandaa mikutano iliyovutia wakazi wengi.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa na uchaguzi wanasema inaonekana wakereketwa kwa Jubilee wameshtushwa na ukweli kwamba vinara wa NASA. wamejitolea kuungana hadi kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

“Suala la kwanza ambalo LIMEVURUGA JUBILEE NA kufanya wapangaji wa mikakati wake kuchunguza upya mipango yao ni kushindwa kutenganisha vinara wa NASA.

Kumbuka kulikuwa na madai kwamba baadhi ya vinara wa upinzani wangejiunga na Jubilee. 

Walipokanusha madai hayo kama propaganda tupu na kutia sahihi mkataba wa kushiriki uchaguzi mkuu pamoja, Jubilee ilitatizika,” alisema mdadisi wa siasa Geoffrey Kamwanah.


Anasema kunyamaza kwa wanasiasa wa Jubilee huku upinzani ukiendelea kuvutia maelfu ya watu katika ngome ambazo zilichukuliwa kuwa za chama tawala kunaonyesha kuna jambo lisilo sawa.

HUENDA KUNA UHUSIANO baridi katika Jubilee yenyewe kwa sababu kwa muda hatujawaona Rais Uhuru na Naibu Wake pamoja hadharani kama ilivyokuwa hapo awali. Hata wakati wa kampeni za kuhamasisha watu kujisajili kupiga kura, kila mmoja alikuwa akifuata njia yake,” akasema.

Takwimu

Mdadisi huyo anahisi kwamba huenda mipango ya Jubilee ilivurugika takwimu za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka zilipoonyesha kwamba hakuna tofauti kubwa katika idadi ya wapigakura katika ngome zake na za NASA.

“Katika hali kama hii, kuna haja ya kubadilisha mikakati ili kuwakabili wapinzani vilivyo. Hata hivyo, wimbi la NASA linavuma kwa nguvu hivi kwamba Jubilee wasipokuwa waangalifu litawasomba,” alisema.

“Uwezekano wa kuwepo kwa uhusiano baridi katika Jubilee unachangiwa na kimya cha watetezi sugu kama vile kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale na Seneta wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen,” aongeza.

Bw Duale na Bw Murkomen walikuwa wanachama wa chama cha United Republican Party URP cha Naibu Rais William Ruto kabla ya vyama tanzu vya muungano wa Jubilee kuvunjwa kuunda chama cha Jubilee.

Kulingana na mdadisi wa siasa Derrick Rono, kuna tetesi kwamba ubaridi uliopo katika Jubilee umechangiwa na hatua ya Rais Kenyatta kunyooshea mkono mwenyekiti wa Kanu Gedion Moi bila baraka za Naibu wake Ruto. Bw Moi na Bw Ruto wamekuwa wakipigania ubabe wa kisiasa eneo la Rift Valley lililo ka kura nyingi.

Chanzo cha uhasama

Japo Kanu kiliunga Jubilee kwenye uchaguzi mkuu uliopita, kilikataa kumezwa na chama cha Jubilee na uhasama ukazidi kati ya Gideon aliye seneta wa Baringo na Naibu Rais William Ruto. Tangu hatua za mwanzo za kubuniwa kwa NASA, kulikuwa na ishara kwamba Kanu ingeunga upinzani.

Ilibidi Rais Kenyatta kukutana na Rais Mstaafu Daniel Moi nyumbani kwake Kabarnet Gardens kwa kile kilichoonekana kumtaka amshawishi mwanawe Gedion kumuunga mkono kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Wadadisi wanasema ni mkutano wa Rais Uhuru ni Mzee Moi ambao ulijiri wiki moja baada ya Mama yake Ngina Kenyatta kukutana na rais huyo wa pili wa Kenya uliozua uhusiano baridi kati ya viongozi wa Jubilee.

“Hisia za Bw Ruto na washirika wake ni kwamba rais alimpuuza naibu wake kwa kuwasiliana na mahasidi wake wa siasa eneo la Rift Valley.

Kumbuka pia Bw Ruto amekuwa akikosoa familia ya Mzee Moi kwa kutaka kuthibiti SIASA ZA RIFT Valley akitaka Gedion kumuunga mkono jinsi yeye( Ruto) alivyomuunga baba yake Mzee Moi,” akasema.

Ruto hana raha

“Kwamba baada ya Rais kukutana na Mzee Moi Kanu ilitangaza kumuunga Rais Kenyatta kwa kipindi cha pili ni hatua ambayo haikumfurahisha Bw Ruto,” asema .

Japo hajazungumzia suala hilo tangu Kanu itangaze itakuwa na wagombezi katika nyadhifa zote isipokuwa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, wandani wa Bw Ruto wanasema angali Jubilee.

“Kwa sasa tuko Jubilee. Hata hivyo, kufuatia matukio ya hivi majuzi, tumeamua kutulia kwa muda kupanga kampeni zetu,” alisema mwandani wa KARIBU WA NAIBU Rais ambaye aliomba tusitaje jina lake kwa sababu sio msemaji wake rasmi.

Anakiri kwamba Bw Ruto hakufurahishwa na hatua ya Kanu kuwa na wagombea urais wake kwenye uchaguzi mkuu ujao japo kinamuunga Rais Kenyatta.

Baadhi ya watetezi wa Jubilee wanasema chama hicho kimefanya kampeni ya kutosha kupitia miradi ya maendeleo tofauti na upinzani ambao hauna cha kujivunia.

Bw Duale anasema umati unaohudhuria mikutano YA KISIASA ya NASA haumaanishi ni kura kwa upinzani.

“Watu ambao hawana mgombea urais wanaweza kushindana nasi tunaojua kwamba Rais Kenyatta na Naibu Wake Ruto watatea kiti chao? Wateua mgombea urais wao na tutajua kwamba wako makini na uchaguzi huu,” akasema Bw Duale.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako