If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, March 27, 2017

KURA KUAMUA KAMA KWELI JOHO NI SULTANI

Na MWAKERA MWAJEFA

IWAPO kura ya utafiti wa kampuni TIFA ni ya kweli, basi gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho, yuko kifua mbele kutetea wadhifa alioushinda kwa kura nyingi kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2013.

Ali Hassan Joho
GAVANA wa Mombasa, Ali Hassan Joho awahutubia wafuasi wake mjini Mombasa baada ya kurejea nchini kutoka Amerika Machi 5, 2017.

Wakati huo, Bw Joho ambaye sasa anafahamika kwa jina la 'Sultan’ alizoa kura 132,507 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Bw Suleiman Shahbal aliyepata kura 94,918.

Wawili hao huenda wakakutana tena debeni Agosti 8, isipokuwa sasa hivi mazingira yamebadilika. Bw Shahbal wakati huo aliwania kupitia chama cha Wiper, lakini sasa amepata tikiti ya moja kwa moja ya chama cha Jubilee.

Ikizingatiwa kuwa aliyekuwa wa tatu, Bw Abdallah Mwaruwa alipata kura 4,739, wengi wanatazama kwa karibu kuona kama kura alizopata Bw Shahbal atazipata au zitaenda kwa Seneta Hassan Omar, ambaye ametangaza kuwania ugavana kupitia chama hicho cha Wiper.

Bw Omar ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho cha Wiper, kwanza atatakiwa kumaliza kibarua cha kupambana na mbunge wa Nyali, Bw Hezron Awiti, kabla ya jina lake kuwa debeni. Huu utakuwa mpambano wa Katibu Mkuu na Mweka Hazina, ambapo lazima mmoja wao alambishwe sakafu.

Kwa upande wa Chama-tawala cha Jubilee mzozo uliokuwa ukitokota baina ya makundi mawili hasimu ya kiongozi na aliyekuwa Mbunge wa Kisauni Anania Mwaboza na mwanabiashara Suleiman Shahbal yalitiwa shwari baada ya vigogo kutoka Nairobi kuingilia kati.


Hata hivyo, bado kuna malalamiko kwa baadhi ya wafuasi wa Jubilee kwamba timu ya Shahbal-Mwaboza ni dhaifu sana kukabiliana na malibwende na majamnajamna ya Gavana Joho kutetea kiti chake.

“Bila ya kumchukua gavana jicho kwa jicho au shilingi kwa shilingi Jubilee itakuwa na kibarua kigumu kumbigija na kumtia adabu kisiasa,” akasema mwandani wa Jubilee ambaye alitaka jina lake libanwe kwa kuogofya lawama.

Tishio la Joho kung’atuliwa mamlakani ni kutoka kwa Chama chaWiper ambacho umaarufu wake unazidi kukua na kusambaa kila pembe ya jimbo la Pwani kwa sababu ya wagombea wengi wa ODM kutilia shaka kura za mchujo za chama hicho.

Wengi wanaofuatilia siasa za Mombasa kutoka bara wanadhani Gavana Joho hana mpinzani wa kumtisha lakini wafuasi wa muungano wa NASA wanaoishi hapa (Mombasa) wana dhana tofauti kabisa na zile za wenzao wa kutoka bara.

Jamii za Kiluo na Kiluhya mtawalia tayari zimeshatoa malalamiko yao kwa vinara wao wa ODM (Raila Odinga), ANC (Musalia Mudavadi) na Ford Kenya (Moses Wetangula) jinsi wanavyodhulumiwa chini ya tawala ya Joho.

Mwakilishi wa Wodi ya Kongowea Jabess Oduor anaonya kuwa iwapo Joho ataachwa kuwa msimamizi mkuu wa mchujo wa ODM, kuna hatari ya chama hicho kupoteza umaarufu Pwani.

“Tayari wafuasi wengi wa chama wametilia shaka mchujo sababu ya tetesi kuna orodha ya wagombeaji washaahidiwa tikiti za moja kwa moja,” akadai Bw Oduor.

Anasema katika miaka minee ya uongozi wa Joho Mombasa, ODM imerudi nyuma.

Kumchafulia jina 

Wapizani wa Gavana Joho wanatarajiwa kutumia ripoti za mkaguzi wa fedha za umma na hadi zake za awali kumchapa viboko na vijembe vya kisiasa ili kuchafulia jina na hadhi yake katika macho ya wapiga kura.

Mathalan, gavana atakuwa na kibarua kigumu kujibu maswali ikiwa ataulizwa kuhusiana na miradi ya vijana iliotengewa Sh100 milioni kujenga vidimbwi vya kufugia samaki katika makasha.

Licha ya kaunti kutumia Sh93, 673,280 ambayo ni asilimia 94 ya mradi wenyewe, mkaguzi wa Fedha hakupata ushahidi wa kuwepo kwa makontena hayo ya kufugia samaki katika wodi zote 30.

Suala jingine nyeti ambalo linatarajiwa kumtoa jasho Bw Joho, ni lile la kuwa na akaunti 22 zinazotumiwa na serikali ya kaunti ambazo wakati wa ukaguzi zilikuwa na salio la Sh193,702,559, bila usawazishaji wowote.

Wapinzani wake pia wanasema kuwa japokuwa Bw Joho atakumbukwa kwa kuwapeleka Mombasa wanamuziki wa kutajika itambidi kueleza ni vipi alilipa Sh90 milioni kwa dakika 90 za tumbuizo la mwanamuziki Chris Brown katika tamasha ambayo haikuzaa mapato yoyote kwa kaunti.

Mapendeleo

Wapinzani hao wakiongozwa na Seneta Omar, wamekuwa wakidadisi mno masuala yanayohusu utumizi wa pesa na utoaji wa tenda, wanaodai unafanywa kwa njia ya mapendeleo.

Kwa mfano Bw Omar anadai kuwa tenda ya ukusanyaji takataka ilipeanwa bila kuzingatia sheria, jambo analosema linachangia kutapakaa uchafu kila mahali mjini Mombasa.

Bw Joho anaandamwa na serikali, na kuna ripoti za kufungiwa baadhi ya akaunti zake za kibinafsi. Hata hivyo, kinachotazamwa na wengi ni jinsi atakavyoteua mgombea mwenza, ikizingatiwa kuwa naibu wake, Bi Hazel Katana amehamia Jubilee, akitaka useneta.

Bi Katana anayetoka jamii ya Mijikenda, iliyo na asilimia kubwa zaidi ya wapiga kura wa Mombasa, anadhaniwa kuchangia kura alizopata gavana huyo. Je, atamteua Mmijikenda mwingine? Ni nani na atakuwa na ushawishi kiasi gani?

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako