If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, March 24, 2017

Kwa mara ya kwanza, ICC kuwalipa fidia wahanga wa jinai za kivita Kongo

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ( ICC) leo Ijumaa imeamuru kuwa kila mmoja kati ya wahanga 297 wa Germain Katanga, mbabe wa zamani wa kivita wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alipwe fidia ya dola 250 kutokana na mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa kijijini kwao mwaka 2003.

Ikiwa ni ishara ya fidia kwa wahanga hao kwa maafa waliyopata kwa ujumla, mahakama ya ICC yenye makao yake mjini The Hague huko Uholanzi imebaini pia kwamba Katanga anawajibishwa kwa maafa jumla ya mali, ya kisaikolojia na kimwili ya dola milioni moja.

Germain Katanga alihukumiwa na mahakama ya ICC kifungo cha miaka 12 jela mwaka 2014, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matano ya jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu kufuatia mashambulizi ya kikabila yaliyofanywa katika kijiji cha Bogoro mkoani Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwezi Februari mwaka 2003.

Germain Katanga, mbabe wa zamani wa kivita Kongo

Katanga pia alituhumiwa kuwapatia silaha wanamgambo katika shambulio ambapo watu 200 waliuliwa kwa kupigwa risasi na kukatwa kwa mapanga.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako