If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, March 13, 2017

Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wakimbilia Sudan

Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wamekimbilia Sudan kutokana na matatizo mengi yanayoikabili nchi yao ukiwemo ukame.

Mtandao wa habari wa al Yaum al SabĂ­ umeripoti habari hiyo na kunukuu taarifa ya ubalozi wa Sudan Kusini mjini Khartoum ukisema kuwa, takwimu za awali zinaonesha kwamba karibu watu 35 elfu wameingia nchini Sudan kutokea Sudan Kusini kwa sababu ya ukame.

Ubalozi huo umesema, msafara wa misaada ya chakula umetumwa Sudan Kusini kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wanaokabiliwa na hali mbaya ya ukame.

Machafuko na uasi umeiletea hasara kubwa nchi changa ya Sudan Kusini

Kitengo cha takwimu cha Sudan Kusini kwa mara ya kwanza kimekiri kuwa vita vya ndani vya miaka mitatu sasa nchini humo vimepelekea kuzuka ukame mkubwa katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Unity.

Karibu nusu ya wananchi wa Sudan Kusini wanahitajia misaada ya dharura ya chakula na madawa, na wanaishi katika ukosefu mkubwa wa usalama.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako