If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, March 6, 2017

Magufuli atoa siku 7 Dangote apewe eneo

NA BASIL MSONGO

RAIS John Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini impe mfanyabiashara Aliko Dangote eneo la kuchimba makaa ya mawe na agizo hilo liwe limetekelezwa ndani ya siku saba kuanzia leo.

Ameiagiza kuwa, makaa ya mawe yakiisha kwenye eneo atakapopewa Dangote, apewe eneo lingine. Ametoa maagizo hayo leo mkoani Mtwara kabla ya kuzindua magari 580 ya Dangote yatakayokuwa yakibeba saruji kutoka kiwandani.

“Nia yangu nataka kiwanda hiki kifanye kweli ili ikiwezekana ujenge viwanda vingine…ujenge hata kumi” amesema Rais Magufuli.

Amemruhusu Dangote auze makaa hayo kwa watu wengine ili Serikali ipate fedha.

Ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kukusanya mapato ya uchimbaji wa makaa hayo kwa Dangote mwenyewe.

Rais amemhakikishia Dangote kuwa, ndani ya siku saba atakuwa amepata kibali cha kuchimba makaa ya mawe kwa ajili ya kiwanda cha saruji kilichopo Mtwara.


Ameiagiza menejimenti ya kiwanda cha Dangote iwasiliane na serikali moja kwa moja badala ya kupitia kwa watu wengine.

Rais amesema, dunia inakwenda haraka sana hivyo uamuzi kuhusu changamoto zilizopo lazima ufanywe haraka ili Tanzania iendane na kasi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako