If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, March 28, 2017

Makumi ya wahajiri haramu watiwa nguvuni Libya wakijaribu kuingia Ulaya

Askari wa kikosi cha Gadi ya Pwani ya Libya wamewatia nguvuni wahajiri haramu 60 wenye uraia wa Bangladesh ambao walikuwa wanajaribu kuingia barani Ulaya kupitia Bahari ya Mediterranean.

Msemaji wa askari wa kikosi cha jeshi na Majini nchini Libya, Ayob Qasim amesema kuwa, askari wa Gadi ya Pwani wamewatia mbaroni wahajiri hao katika mji wa Zawiyah, magharibi mwa Tripol. Amesema kuwa wahajiri hao wamepelekwa katika bandari ya mji wa Zawiyah na kukabidhiwa kwa maafisa wa Idara ya Kupambana na Wahajiri Haramu.

Kutokana na Libya kushindwa kudhibiti mipaka yake sambamba na uhaba vitendea kazi na fedha wa kikosi cha ulinzi ya pwani unaosababishwa na machafuko ya ndani, nchi hiyo imekuwa daraja la makundi ya wahajiri haramu wanaoelekea barani Ulaya ambao wanadhania watapata maisha bora na ajira. Wahajiri hao hutumia pwani ya Libya yenye urefu wa karibu kilometa 300 kwa ajili ya kuelekea katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.

Wahajiri haramu wakiwa mbioni kuelekea Ulaya

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) karibu wahajiri laki tano na 15 elfu wamevuka Bahari ya Mediterranean kuingia Ulaya tangu mwanzoni mwa mwaka huu pekee na karibu 3000 miongoni mwao wamepoteza maisha katika harakati hizo.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako