If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, March 25, 2017

MARWA AAMURU JUBILEE WASIANDAE MKUTANO MVITA

Na GALGALO BOCHA

MSHIRIKISHI wa usalama kanda ya Pwani, Nelson Marwa ameagiza kufutilia mbali mkutano wa kisiasa wa chama cha Jubilee uliopangwa kufanyika Jumapili katika uwanja wa Mvita.

Nelson Marwa
Mshirikishi wa eneo la Pwani Nelson Marwa. Picha/MAKTABA

Marwa alisema Jumamosi kuwa hatua ya kuzima maandalizi ya mkutano huo ilitokana na sababu za kiusalama.

Marwa alisema chama cha ODM ndicho cha kwanza kuarifu polisi kuanda mkutano wao wa Jumapili katika uwanja wa Tononoka.

Kinara wa ODM Raila Odinga amewasili Mombasa kwa ajili ya mkutano wa kesho Jumapili.

“Majuzi ODM walipotaka kufanya mkutano sambasamba na ule wa Jubilee katika uwanja huo, tulizungumza nao na wakakubali kuusitisha. Leo hii tunachukua uamuzi wakati huu kueleza Jubilee kukomesha mkutano wao maana ODM ndiyo walitangulia kuarifu polisi,” akaeleza Marwa.

Alisema NASA na Jubilee hawataruhusiwa kuonyeshana ubabe na ushindani kwa kuandaa mikutano sambasamba ya kisiasa katika majukwaa yaliyokaribiana.

“Uwanja wa Tononoka na Mvita ni pua kwa mdomo. Waelewa changamoto ya kiusalama. 

Hatutaruhusu wanasiasa kupanda mbegu ya ghasia kwa kuandaa mikutano kama hayo. Wakitaka waende Kilifi, Malindi au Kwale wafanye yao,” akaeleza Marwa.

Alivitaka vyama vya kisiasa kushirikiana na vyombo vya kiusalama katika maandalizi ya mikutano ya kisiasa.


“Hatutakubali maandalizi ya mikutano ya kisiasa isiyokuwa na mipangilio. Wakati kampeni zitakapoanza ramsi, wawe tayari kufanya hata mikutano 100 maana tutaweza kukabili hali lakini si sasa,” akaeleza Marwa.

Naye Msemaji wa polisi, Erick Kiraithe alisema wanasiasa hawapaswi kufanya mikutano kwa ajili ya kuleta vurugu na ghasia.

Akizungumza na wanahabari katika Mbaraki Sports Club, Mombasa, Kiraithe aliunga mkono hatua ya polisi ya kuzima mkutano wa Magavana Hassan Joho (Mombasa) na Amason Kingi (Kilifi) mjini Kinango, kaunti ya Kwale.

“Kama kuna mkutano halali na wanaohudhuria mkutano huo, kwa wakati mmoja, watatekeleza jambo ambalo laweza kusababisha uvunjaji wa kisheria, basi polisi hawatasita kuchukua hatua licha uhalali wa mkutano kama huo,” akaeleza Kiraithe.

Aidha alisema serikali kuu ina Imani kubwa kwamba Bw Marwa atasimamia ipasavyo usalama wa kanda ya Pwani na serikali kuu kuingilia panapohitajika.

Afisa mmoja wa mawasiliano katika halmashauri kuu ya chama cha Jubilee Pwani, alisema wamesikitishwa na uamuzi wa Bw Marwa kusitisha mkutano wao.

Hata hivyo, alisema “wamekubaliana kutofanya mkutano huo kwa vile wao ni raia wanaotii sheria”
“Hata hivyo kuna mambo yanayostahili kutatuliwa lakini tutatafuta nafasi nyingine ili kutangaza,” akaeleza afisa huyo faraghani.

Source: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako