If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, March 26, 2017

Mataa yazimwa kwa saa moja duniani kulinda mazingira

Miji ya nchi 170 duniani, ikiwemo Iran imeshiriki kwenye zoezi la kuzima taa kwa muda wa saa moja jioni ya tarehe 25 Machi.

Zoezi hilo lilianzishwa mwaka 2007 kwa lengo la kuwahamasisha walimwengu watumie mbinu mbalimbali za kupunguza utoaji wa hewa zinazoweza kusababisha kupanda kwa joto duniani, kubana matumizi ya nishati na kuhifadhi mazingira.

Ikiwa ni mara ya kumi, Jumamosi jioni, watu kila mahali walishiriki katika "saa moja ya kujali mazingira ulimwenguni" kama ishara ya kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Katika ujumbe wake kuhusu tukio hilo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuhatarisha maisha na vipato duniani kote. 

Ameongeza kuwa, mwaka jana ulikuwa tena mwaka uliovunja rekodi ya juu zaidi ya joto. Aidha amesisitiza kuwa Mkataba wa Paris unatupa fursa ya kipekee ya kuzuia kupanda kwa kiwango cha kimataifa cha joto, kukuza nishati safi kwa wote na kujenga mustakabali endelevu.

Mnara wa Azadi pamoja na ule wa Milad jijini Tehran ilizimwa taa kwa mnasaba wa 'saa moja ya kujali mazingira duniani'


Vile vile ametoa wito kwa serikali na sekta binafsi kwamba ni lazima zifanya juhudi kubwa zaidi kama ambavyo pia amewataka watu binafsi nao wafuate mkondo huo. Amesema jukumu la kuijenga kesho iliyo endelevu, ni la kila mmoja wetu leo hii.

Kwa mnasaba huo maeneo mashuhuri kama vile Mnara wa Milad na Medani ya Azadi mjini Tehran ilizimwa taa kama njia ya Iran ya kujiunga na mataifa mengine duniani kulinda mazingira.

1 comment:

  1. It’s so valuable I information to give me, If you want to know properties in Hyderabad/Vijayawada please check property information Ramky Estates & Farms Limited
    Announce a New Project "Tranquillas" Located at Nallagandla, Gachibowli, Hyderabad.
    4 BHK Villas for sale in Gachibowli
    Ramky Tranquillas

    ReplyDelete

Maoni yako