If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, March 18, 2017

Mazungumzo yasiyo na natija kati ya Merkel na Trump

Rais Donald Trump wa Marekani na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel jana alasiri Machi 17 walifanya mazungumzo katika ikulu ya Rais wa Marekani (White House). Mazungumzo hayo yameshindwa kupunguza hitilafu za pande mbili katika masuala ya uchumi, usalama, siasa na jamii kutokana na viongozi wa Ujerumani na Marekani kushikilia misimamo yao ya huko nyuma.

Ujerumani inahitilafiana na serikali ya sasa ya Marekani kuhusu mambo mengi kuanzia biashara ya kimataifa hadi gharama za kiulinzi, mikataba ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kadhia ya wakimbizi.

Baada ya Donald Trump kushika hatamu za uongozi tarehe 20 mwezi Januari mwaka huu na kutoa matamshi na misimamo iliyoibua makelele na upinzani kuhusu masuala mengi ya Ulaya hususan mustakbali wa NATO, mwenendo mbaya wa Trump mkabala na Umoja wa Ulaya, hali ya mkataba wa bishara huru kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani na misimamo mikali wa Trump katika kadhia ya wahajiri na wakimbizi, yote hayo yameufanya uhusiano wa kirafiki wa pande mbili hizo za Antlantic kukumbwa na mikingamo mingi.

Ujerumani ikiwa ni nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya na mwanachama muhimu wa Umoja wa Ulaya imekumbwa na wasiwasi mkubwa kuhusiana na masuala mawili yanayohusiana na mwelekeo wa kibiashara na kiuchumi ya serikali mpya ya Marekani na vilevile misimamo ya kiukosoaji ya serikali ya Trump kuhusu NATO na Umoja wa Ulaya.

Katika upande mwingine, Bi. Angela Merkel ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi waliopendekeza na kuunga mkono sera za milango wazi katika kuamiliana na wakimbizi, anashangazwa na siasa za Trump katika uwanja huo ambaye amechukua msimami unaopingana kikamilifu na ule wa Merkel kuhusu mgogoro wa wakimbizi.

Trump anaamini kuwa, suala la kukubaliwa uhajiri ni msaada na si haki na kwa msingi huo anaamini kuwa, usalama wa raia wa Marekani unapewa kipaumbele zaidi. Angela Merkel anapinga mtazamo huo na anakosoa dikrii iliyotolewa na Donald Trump inayowazuia raia wa nchi sita za Kiislamu kuingia Marekani.

Bi Angela Merkel Kansela wa Ujerumani katika mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani

Kwa kuzingatia masuala hayo yote ilitazamiwa tangu huko nyuma kuwa mazungumzo kati ya viongozi hao wa Ujerumani na Marekani hayatakuwa mapesi wala ya kirafiki. Pamoja na hayo, kabla ya mazungumzo hayo ya jana, Merkel alitamka kuwa anataka kufanya mazungumzo ya kiadilifu na kufikiwa makubaliano yenye faida kwa pande zote.


Moja ya mambo yanayoitia wasiwasi Ujerumani kuhusu siasa za biashara na uchumi za serikali ya Trump na jitihada za kiongozi huyo Marekani za kuweka vizuizi vya kiuchumi na kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo.

Kwa kuzingatia kuwa Ujerumani ni nchi inayoshika nafasi ya kwanza kati ya nchi zinazouza bidhaa nchini Marekani kati ya nchi za Ulaya, habari hii haiwafurahishi viongozi wa Berlin. Kabla ya mazungumzo ya Merkel na Trump, Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Brigitte Zypries alieleza kuwa nchi hiyo huenda ikawasilisha malalamiko yake dhidi ya Marekani katika Shirika la Biashara Duniani (WTO) kutokana na pendekezo lililowasilishwa na Trump la kutaka kutozwa kodi za mpakani bidhaa zinazoingizwa nchini.

Brigitte Zypries, Waziri wa Uchumi wa Ujerumani

Kuhusiana na suala hilo, viongozi wa Ujerumani wana wasiwasi wa kuidhinishwa ushuru mkubwa wa forodha wa asilimia 35 kwa magari ya nchi hiyo yanayoingizwa katika masoko ya Marekani ambayo yanatengenezewa huko Mexico. Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa sheria za Shirika la Biashara Duniani, ni marufuku kuidhinishwa nyongeza ya kodi ya magari kutoka nje kwa zaidi ya asilimia 2.5.

Kuhusiana na kadhia nyinginezo muhimu yaani mustakbali wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) pia Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel ameaidi kuzidisha gharama za masuala ya ulinzi ya nchi hiyo kwa asilimia mbili ya uzalishaji ghafi (GDP) hadi mwaka 2024 na kusisitiza kuwa, bajeti ya kijeshi ya Ujerumani iliongezeka kwa asilimia nane mwaka jana wa 2016 ikilinganishwa na miaka ya huko nyuma. Hata hivyo Rais Donald Trump wa Marekani angali anatilia mkazo msimamo wake juu ya udharura wa kushiriki vilivyo waitifaki wa Ulaya wa nchi hiyo katika kuudhamini fedha za bajeti ya Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi.

Moja kati ya masuala muhimu yaliyojadiliwa jana mjini Washington kati ya Merkel na Trump ni kuhusu mustakbali wa uhusiano na Russia. Kwa kuzingatia wasiwasi walionao viongozi wa Ulaya kuhusu uwezekano wa kuboreka uhusiano kati ya Marekani na Russia, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel kwa mara nyingine tena amesisitiza kwamba japokuwa uhusiano wa nchi za Magharibi na Moscow unapasa kuboreka, lakini suala hilo litategemea kutekelezwa makubaliano ya Minsk na kupatiwa ufumbuzi mgogoro wa Ukraine. Kwa msingi huo, Merkel kwa mara nyingine tena amesisitiza msimamo mmoja wa Ulaya kuhusiana na kadhia ya Moscow na kupinga hatua yoyote ya upatanishi wa Washington katika uwanja huo.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako