If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, March 3, 2017

MTUHUMIWA WA BANGI AFA GHAFLA MAHAKAMANI

Na PHINIAS BASHAYA  BUKOBA, TANZANIA

MSHATAKIWA anayekabiliwa na tuhuma za kukamatwa madebe mawili ya bangi amekufa ghafla alipoitwa wakati jalada la kesi dhidi yake lilipokuwa likipelekwa mbele ya hakimu.

Kudra Winchislaus
Wananchi wakiangalia mwili wa Kudra Winchislaus aliyeanguka na kuaga dunia wakati akisubiri kusikiliza shauri lake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Bukoba Machi 2, 2017. Picha/PHINIAS BASHAYA

Umato ulimwona mshtakiwa Kudra Winchislaus ambaye alikuwa nje kwa dhamana, akiwa ameanguka Alhamisi alipokwenda kusikiliza kesi yake katika mahakama ya Wilaya ya Bukoba.

Taarifa zilisema Kudra ambaye ni mkazi wa Kata ya Kibera mjini Bukoba alikuwa akikabiliwa na shtaka la kukamatwa na madebe mawili ya bangi katika kesi Na. 58 iliyofunguliwa mahakamani hapo tangu mwaka 2016.

Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Kilwanila Kiiza akizungumza kwa simu jana alithibitisha kupokewa mwili wa mwanamke huyo mwenye miaka 36.

Tukio hilo limeibua mjadala kwa watu walioshuhudia tukio hilo na baadhi walisema maisha yake yangenusurika iwapo kungekuwa na ujuzi wa kutoa huduma ya kwanza.

Pia imeibuka hoja ya umuhinu wa watumiaji wa simu kutoweka namba za simu kwenye simu zao, kwa kuwa ilikuwa rahisi kuwapata ndugu zake kupitia simu yake ambayo haikuwa imefungwa kwa namba ya siri

Moja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema ilimchukua muda kabla ya kupoteza maisha mama huyo huku wananchi wakishindwa kujua aina ya huduma sahihi iliyotakiwa kutolewa.


Shuhuda huyo Hamza Mugasha alisema mama huyo alikuwa akipumua kwa nguvu baada ya kesi yake kuitwa huku wananchi wakiishia kumpepea tu.

Mwanasheria wa Serikali Emmanuel Mavela alisema mwanamke huyo alikuwa akikabiliwa na shtaka hilo tangu mwaka 2016 na lilikuwa lianze kusikilizwa mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Samwel Maveda.

“Alipoitwa kusikiliza kesi yake alianguka na kuanza kupatiwa msaada. Alikuwa ameshtakiwa akidaiwa kukutwa na dawa za kulevya, madebe mawili ya bangi. Ni shauri Namba 58 lililofunguliwa katika mahakama hii tangu mwaka jana,” alisema Mavela.

Tukio hilo lilisababisha taharuki kwa wafanyakazi na wananchi waliokuwa katika viwanja vya mahakama hiyo, ambao walikusanyika ulipokuwa mwili wa mwanamke huyo. Baadaye ulifunikwa na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.

Kufafanua

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Augustino Olomi alisema alipata taarifa za tukio hilo na kwamba angetoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari baadaye kwa kuwa alikuwa Uwanja wa ndege wa Bukoba kwa ajili ya mapokezi ya Mkuu wa Majeshi nchini.

Baadhi ya sababu zinazotajwa na wataalamu wa afya kwamba zingeweza kuwa sababu ya kifo cha mama hiyo ni mapigo ya moyo kuwa chini au juu, mshtuko, kukata tamaa na kuwa na mawazo kupitiliza.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako