If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, March 12, 2017

RAIS KENYATTA AKARIBISHA DAN MWAZO, LAY KATIKA JP

Na LUCY MKANYIKA

RAIS Uhuru Kenyatta amepiga kambi katika eneo la Pwani kupigia debe chama cha Jubilee.

Rais aliongoza viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo Naibu Rais Wilkiam Ruto na mawaziri wake katika msururu wa ziara ya kuzindua miradi mbalimbali katika eneo hilo linalosifika kuwa ngombe ya upinzani.

Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta azungumza na Askofu Martin Kivuva wa Kanisa Katoliki, Mombasa alipohutubia wakazi wa Bura. Picha/PSCU

Katika ziara yake katika kaunti ya Taita Taveta mnamo Jumamosi, Rais Kenyatta alizindua ujenzi wa barabara ya Bura Mission katika Kaunti ndogo ya Mwatate.

Vilevile, Rais Kenyatta alikagua ujenzi wa barabara ya Voi-Wundanyi na ujenzi wa Taasisi ya Madini katika chuo kikuu cha Taita Taveta.

Akiongea katika eneo la Bura Mission, Rais Kenyatta alishutumu vikali viongozi wa upinzani kwa kudai kuwa serikali imefeli kufanya maendeleo nchini.

“Tumefanya miradi mbalimbali si hapa Taita Taveta tu bali pia katika sehemu zote nchini. Wanaodai kuwa hakuna kitu tumefanya wanapotosha wananchi,” akasema.

Rais aliwasuta wanaomshambulia kwa kutumia matamshi makali dhidi ya viongozi aina hiyo.

“Viongozi ambao wanadanganya wananchi kuhusu hii serikali wanafaa kuitwa majina kama hayo,” akasema.

Wakati huohuo, Seneta Dan Mwazo alikihama chama cha ODM na kujiunga na Jubilee Party.


Mwazo na Bi Joyce Lay wamelakiwa rasmi katika chama hicho na Rais Kenyatta na naibu wake katika mkutano wa hadhara wa leo Jumamosi mjini Voi.
Mwazo na Bi Lay watatumia chama hicho kuwania nyadhifa za ugavana na useneta mtawalia.

“Serikali hii imeleta maendeleo mengi katika eneo hili ndio maana nimeamua kuunga mkono serikali ya Kenyatta,” akasema Mwazo.
Vilevile Rais anatarajiwa kukagua ujenzi wa jumba la madini mjini Voi.

Jumapili, Rais anatarajiwa kuongoza msafara huo kufanya mkutano mkubwa wa kisiasa katika uwanja wa Tononoka jijini Mombasa.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako