If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, March 10, 2017

Rais wa Korea Kusini aondolewa madarakani

Mahakama ya kikatiba ya Korea Kusini imetoa uamuzi wa kuufikisha mwisho utawala wa Rais Park Geun hye aliyeshitakiwa na bunge la nchi hiyo. Hatua hiyo inakuja kufuatia mgogoro wa kisiasa uliolitikisa taifa hilo la Asia.

Südkorea Park Geun-Hye (Getty Images/AFP/J. Heon-Kyun)
Südkorea Park Geun-Hye (Getty Images/AFP/J. Heon-Kyun)

Bunge lilimshitaki Park mwezi Desemba kwa kutumia vibaya madaraka na ufisadi baada ya mamilioni ya watu kuandamana wakimtaka rais huyo ajiuzulu kufuatia kashfa mbalimbali za ufisadi na rushwa. Uamuzi huo uliofikiwa na jopo la majaji wanane wa mahakama ya kikatiba ambao hauwezi kukatiwa rufaa unamaanisha Korea Kusini itafanya uchaguzi katika kipindi cha miezi miwili ijayo kumchagua rais mpya.

Inamaanisha pia Park, mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo anakuwa kiongozi wa kwanza kuondolewa madarakani baada ya kushitakiwa na bunge, kupoteza kinga ya rais iliyokuwa ikimlinda dhidi ya kufunguliwa mashitaka. Jaji Mkuu wa mahakama hiyo ya kikatiba Lee Jung Mi amesema vitendo vya Park vilihujumu vibaya sheria na demokrasia.

Urafiki wamchongea

Park mwenye umri wa miaka 65 alikutwa na hatia ya kuvunja sheria kwa kumruhusu rafiki yake Choi Soon Sil kuingilia masuala ya kitaifa na kukiuka sheria kuhusu shughuli za utumishi wa umma. Park anadaiwa kuficha uingiliaji huo uliofanywa na Choi na hata kuwashutumu walioyaibua madai hayo.
Südkorea Prozess Choi Soon-sil (picture-alliance/AP Photo)

Südkorea Prozess Choi Soon-sil
Choi Soon sil rafiki ya Rais Park

Kwon Seong Dong mbunge na mwanachama wa kamati ya bunge ya mashitaka amesema uamuzi huo wa mahakama unathibitisha kuwa kila mtu ni sawa mbele ya sheria, hata rais. Park binti wa kiongozi wa zamani wa kiimla aliyeungwa mkono na jeshi la nchi hiyo aliingia madarakani mwaka 2012 baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa kidemokrasia.

Endelea kusoma zaidi: dw.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako