If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, March 23, 2017

Rais wa Tanzania amfuta kazi Nape Nnauye

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania leo Alkhamisi amefanya mabadiliko mengine katika Baraza la Mawaziri.

Taarifa ya Ikulu ya Tanzania imesema kuwa, katika mabadiliko hayo, Rais Magufuli amemteua Dk Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na kada maarufu wa chama tawala cha CCM, Nape Nnuaye. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mabadiliko mengine yaliyofanywa leo na Rais wa Tanzania ni kumteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Hata hivyo taarifa hiyo ya Ikulu ya Tanzania haikutaja hatima ya waziri wa zamani wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, bali imesema tu kuwa uteuzi huo unaaza mara moja na wateule hao wawili wataapishwa kesho Ijumaa mchana Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania

Ikumbukwe kuwa jana Nape Nnauye alipokea ripoti ya tume aliyounda kwa ajili ya kuchunguza uvamizi uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, katika majengo ya Clouds Media Group, uvamizi ambao umelalamikiwa vikali na duru mbalimbali hususan vyombo vya habari vya Tanzania.


Baada ya kupokea ripoti hiyo yenye mapendekezo kadhaa mazito, Nnauye alisema ataiwasilisha kwa wakubwa wake, Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania kwa ajili ya kuchukuliwa maamuzi. 

Miongoni mwa mapendekezo ya tume hiyo ni pamoja na Waziri Nape Nnauye awasilishe rasmi malalamiko ya tasnia ya habari dhidi ya Makonda.

Vyombo vya dola viwachunguze askari walioingia na bunduki kwenye kituo cha televisheni pamoja na kampuni ya Clouds Media kupitia upya miongozo, kanuni, sheria na taratibu ili kudhibiti watu wasiohusika kuingia kwenye chumba cha habari.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako