If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, March 22, 2017

SENETA AWASHTUKIA MADIWANI KUSHINIKIZA MALIPO BILA KAZI

Na MOHAMED AHMED

SENETA wa kaunti ya Makueni, Mutula Kilonzo Jnr amekejeli ombi la madiwani kutaka kufidiwa miezi minane ambayo hawatakuwa ofisini.

Mutula Kilonzo Jn
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Kuangazia Katiba, Mutula Kilonzo Jnr ahutubu kwenye kikao cha Juni 25, 2015 katika majengo ya Bunge. Picha/DIANA NGILA

Kilonzo alisema ombi hilo la viongozi hao ni 'haramu na kinyume na sheria'.

Alisema kuwa kulingana na maelezo ya Katiba, hakuna kifungu cha sheria kinachowapa nafasi viongozi hao 'kujiliwaza kwa malipo bila kazi' tofauti na viongozi wenzao.

“Tuliwekwa kwenye kikao sisi sote na kuonywa kuwa yeyote yule atakayetaka kupewa mshahara baada ya Agosti 8, 2017 aelewe itakuwa ni kinyume na sheria. Baada ya kuundwa kwa katiba na kukaamulika kuwa tutafanya uchaguzi ilikuwa wazi kuwa yoyote atakayechaguliwa kati ya mwaka 2013 na 2017 atakuwa na muhula ambao hatohudumu katika miaka yake mitano,” akasema.

Seneta huyo wa kaunti ya Makueni aliongeza kuwa haiwezekani kwa uchaguzi mkuu wa nafasi za juu kama vile kiti cha gavana kufanyika kisha uchaguzi wa wawakilishi wa wadi ufuatie baadaye.

“Sheria inasema kuwa madiwani wanatakikana ofisini siku 14 baada ya uchaguzi. Hii inaamanisha baada ya uchaguzi wa Agosti 8 lazima tuwe na bunge la wawakilishi wa wadi ofisini,” akaongeza.


Alikuwa akizungumza katika mahojiano na Swahilihub wakati wa warsha ya maseneta na madiwani katika hoteli ya Pride Inn jijini Mombasa.

Aidha, alisema kuwa viongozi hao wamekuwa wakitafsiri vibaya kifungu nambari 177(4) cha Katiba ambacho alisema kuwa kilitafsiriwa zaidi kuwa kutakuwapo na muhula ambao viongozi hawatohudumu katika miaka mitano yao ya uongozi.

Mnamo Jumanne madiwani walitishia kuwa wataghairi kuondoka mamlakani baada ya uchaguzi na kusema kuwa wanastahili kulipwa 'stahili yao ya miezi minane' ndipo wafuate hatua zingine zinazohitajika.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako