If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, March 29, 2017

Shein aahidi kukabili changamoto za elimu

NA MWANDISHI MAALUMU, ZANZIBAR

AIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itaendelea kuchukua juhudi katika kutatua changamoto zote zilizopo kwenye sekta ya elimu hatua kwa hatua.

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akitoa hotuba wakati wa mkutano na walimu wa shule za sekondari za mikoa mitatu ya Unguja, uliofanyika mjini Unguja. (Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akitoa hotuba wakati wa mkutano na walimu wa shule za sekondari za mikoa mitatu ya Unguja, uliofanyika mjini Unguja. (Picha na Ikulu).

Aliyasema hayo wakati alipokuwa na mkutano na walimu wa shule za sekondari kwa shule za mikoa yote mitatu ya Unguja kwenye Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi.

Alisema changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiikabili sekta ya elimu tayari zimeshaanza kufanyiwa kazi na serikali anayoiongoza, hatua ambayo ni uthibitisho kwamba serikali ina dhamira ya dhati katika kuimarisha sekta ya elimu kwa kuzingatia umuhimu kwa maendeleo.

Alisema SMZ itaendelea kutatua changamoto hizo kwa mujibu wa fedha zilizopo serikalini ili kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu 2016/2020, Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015- 2020, Mpango wa MKUZA III na mipango mengine ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa.

Alisisitiza kuwa, serikali itaweka kipaumbele maalumu katika kuimarisha mazingira ya kufanya kazi walimu ili yawe bora zaidi ambapo itahakikisha muundo wa utumishi wa Wizara ya Elimu unafanyiwa kazi ili kila mfanyakazi wakiwemo walimu wapate stahiki zao kwa mujibu wa sifa za kitaaluma, uzoefu na dhamana zao.


Aidha, alisisitiza haja ya kuimarisha uhusiano baina ya walimu na wazazi ili kuongeza ufanisi katika ufaulu wa wanafunzi hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa katika shule nyingi, Kamati za Wazee zimepoteza nguvu na hivyo kushindwa kuwaunganisha wazazi na walimu.

Hivyo, alitoa mwito kwa uongozi wa shule kuziimarisha Kamati za Shule na hata kuwa na siku za wazazi kwa lengo la kuimarisha uhusiano baina ya wazazi na uongozi wa shule.

Pia, Dk Shein alisisitiza haja kwa walimu kuwa na mbinu bora za kufundishia na kuwasaidia wanafunzi, ikiwa ni pamoja na walimu kujiandaa kabla ya kufundisha na pia wawe tayari kujiendeleza kitaaluma na kujifunza kwa wengine wanaofanya vizuri.

Akisisitiza suala la ukaguzi wa shule na walimu.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako