If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, March 20, 2017

SONKO AOMBA RADHI KWA KUTOA CHECHE ZA MATUSI KWA RUNINGA

Na LEONARD ONYANGO

SENETA wa Nairobi Mike Sonko ameomba msamaha baada ya kutoa kauli zilizosheheni matusi alipokuwa akihojiwa na runinga ya Citizen TV, Jumapili usiku.

Mike Mbuvi Sonko
Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko awali. Picha/SALATON NJAU

Bw Sonko ambaye anamezea mate kiti cha ugavana wa Nairobi, hata hivyo, alidinda kumwomba msamaha mshindani wake mkuu Peter Kenneth, ambaye alimiminia cheche za maeneo ya kumdunisha.

Kupitia mtandao wa Twitter, Bw Sonko alijitetea kwamba alitoa maneno ya matusi kwa sababu alikuwa amejawa na ghadhabu.

“Kama niliwajamisha katika jana poleni nilikuwa na hasira my opponent aliniita hooligan in public wenzake wakaniita mbwa ndani ya kanisa.

Ikiwa niliwakera katika mahojiano ya jana naomba msamaha mpinzani wangu aliniita mhuni hadharani huku wenzake wakinirejelea kama mbwa wakiwa kanisani,” akasema Bw Sonko.

Seneta Sonko, hata hivyo, alikataa kuomba msamaha kwa kutoa matamshi ya kuwadunisha watu wenye uelemavu wa ngozi (albino) licha ya kushutumiwa vikali na Wakenya katika mitandao ya kijamii..

Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini na mbunge wa Maalumu Issac Mwaura, alikuwa miongoni mwa Wakenya walimshutumu Bw Sonko kwa kudunisha watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.


“Kutusi watu kwa sababu ya rangi ya ngozi yao ni kukiuka kifungu cha 27 cha katiba ambayo kila seneta anafaa kuheshimu,” akasema Bw Mwaura ambaye pia anamezea mate kiti cha ubunge wa Ruiru.

Bw Mwaura alimtaka Seneta Sonko kuwaomba msamaha watu wenye ulemavu wa ngozi.
Mbunge huyo alisema matamshi hayo ya Seneta Sonko yalilenga kuwadunisha na kuwabagua Albino.

Mbunge huyo Maalumu anayewakilisha masilahi ya walemavu bungeni alikitaka chama cha Jubilee kumchukulia hatua za kinidhamu Bw Sonko kwa kuwadumisha albino.

“Tunahitaji viongozi wanaoheshimu watu wengine. Sonko ni sharti aombe msamaha la sivyo tutamchukulia hatua,” akasema Bw Mwaura.

Alipokuwa akihojiwa na runinga ya Citizen TV, Bw Sonko alimrejelea mbunge wa zamani wa Gatanga Bw Kenneth kuwa ‘albino’.

Seneta huyo alisisitiza kuwa hayuko tayari kufanya kazi na Bw Kenneth huku akimtaka kuomba msamaha Rais Uhuru Kenyatta kwa kumpinga mnamo 2013 alipowania urais.

Bw Sonko pia lidai kwamba Bw Kenneth alijizolea alama ya ‘E’ katika masomo manne kwenye mtihani wa Kidato cha Nne alipokuwa katika shule ya upili ya Starahe.

“Siko tayari kujiondoa katika kinyang’anyiro cha ugavana ili kumpisha PK. Ni heri niunge mkono mwanasiasa mwingine kutoka Murang’a au Mlima Kenya lakini si PK,” akasema Bw Sonko huku akirejelea Peter Kenneth.

Tabia ya Bw Sonko aliyekuwa akizungumza bila kikomo, kutoa cheche za matusi na hata kumkatiza mtangazaji wa runinga ya Citizen TV Hussein Mohammed alipojaribu kuzungumza, iliwakera Wakenya ambao baadaye walielezea hisia zao katika mitandao ya kijamii.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako