If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, March 8, 2017

TRUMP ATAMPIGIA SIMU RAIS KENYATTA?

Na SAMMY WAWERU

KIONGOZI wa taifa, Rais Uhuru Kenyatta anatarijia kupigiwa simu rasmi na Rais wa Marekani, Donald Trump Jumanne Machi 7, 2017 kutoka Ikulu ya White House.

Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump. Picha/AFP

Kulingana na ripoti inayoonyesha ratiba ya Rais Trump kutoka Ikulu ya White House, inafichua mazungumzo ya viongozi hawa wawili kwa simu yatafanyika mwendo saa kumi na mbili na robo za jioni saa za Afrika Mashariki ambazo ni saa nne na robo za asubuhi saa za Marekani Jumanne Machi 7, 2017.

Mazungumzo hayo yatakayochukua takriban dakika 30 yanatarajiwa kuzungumzia jinsi ya kuimarisha hali ya usalama hapa nchini, kukabiliana na makundi ya haramu ya ugaidi, na jinsi mataifa haya mawili, Kenya na US yatakavyoshirikiana kudumisha amani Somalia kando na kujadili kuhusu janga la ukame katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Haya yatajiri baada ya Rais Trump mnamo Februari 13, 2017 kuzungumza na marais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Mohammadu Buhari wa Nigeria kwa simu.

Katika mazungumzo yake na Rais Jacob Zuma, Trump walijadili kuhusu kuboresha na kukuza biashara kati ya Afrika Kusini na Marekani.


Trump na Buhari wa Nigeria walizungumza jinsi ya kuimarisha usalama Afrika Magharibi huku ikikumbukwa kwamba nchi ya Nigeria imekuwa ikikumbwa na kudorora kwa hali ya usalama kwa sababu ya kikundi haramu cha Boko Harram.

Uhuru atakuwa Rais wa tatu kuzungumza na Rais Trump baada ya Jacob Zuma na Mohammadu Buhari, tangu alipochukuwa hatamu ya uongozi kutoka kwa Rais Mstaafu Barrack Obama mwanzoni mwa 2017.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako