If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, March 19, 2017

UHURU AWATEMBELEA KDF WANAOPAMBANA NA AL-SHABAAB

Na PSCU

Rais Uhuru Kenyatta amewatembelea wanajeshi wa Kenya walio chini ya muungano wa majeshi ya Afrika nchini Somalia AMISOM katika kambi ya Dhobley.

Rais Uhuru Kenyatta awapungia wanajeshi wa KDF Jumamosi, Machi 18, 2017 katika kambi ya Dhobley nchini Somalia. Picha/PSCU

RAIS Kenyatta amewatembelea wanajeshi wa Kenya walio chini ya muungano wa majeshi ya Afrika nchini Somalia AMISOM katika kambi ya Dhobley.

Rais Kenyatta aliyekuwa amevalia kijeshi amepongeza KDF kwa kujitolea kuilinda mipaka ya Kenya.

Imekuwa ziara yake ya kwanza kuwatembelea wanajeshi licha ya kuzuru jiji kuu la Mogadishu katika shughuli tofauti rasmi.

"Nawapongeza kwa kujitolea kuingia hapa Somalia kukabiliana na Al-Shabaab. Mmetoa mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya raia wasiokuwa na hatia nyumbani Kenya na hata hapa kwa majirani wetu," amesema Rais Kenyatta.

Rais amesema kwamba anashauriana na serikali ya Somalia iunde jeshi dhabiti la kuilinda nao KDF warejee nchini Kenya.Aidha, amesema vita dhidi ya ugaidi vimesaidia kuimarisha sekta ya utalii nchini Kenya.

Mkuu wa Majeshi, Jenerali Samson Mwathethe amempongeza Rais Kenyatta kuwatembelea wanajeshi.

"Rais bila shaka wanajeshi wameona juhudi zako za kuwapiga jeki na kuwaonyesha ulivyojitolea kuhakikisha magaidi wanatokomezwa," amesema Jenerali Mwathethe.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako