If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, March 23, 2017

UHURU, RAIS WA SOMALIA WASHAURIANA JIJINI NAIROBI

Na PSC

Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo amefanya ziara rasmi nchini Kenya ambapo yeye na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta wamejadili suala la ushirikiano baina ya mataifa haya jirani.

Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo akiwa nchini Kenya na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta Machi 23, 2017 katika Ikulu jijini Nairobi. Picha/PSCU

RAIS mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo amefanya ziara rasmi nchini Kenya ambapo yeye na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta wamejadili suala la ushirikiano baina ya mataifa haya jirani.

Kenyatta na Farmajo kwenye kikao cha majadiliano ya ushirikiano wamesema ni muhimu mataifa haya mawili kuafikia usalama, biashara na uwekezaji, huduma za usafiri wa angani, elimu, zaraa, ugavi wa raslimali, mifugo, uvuvi, utalii, uhamiaji, leba na afya.

Farmajo aliyechaguliwa Rais Februari 8, 2017, amepokelewa Alhamisi kwa taadhima kuu na akapokezwa heshima za kijeshi ambapo pia alilikagua gwaride la heshima katika Ikulu ya Nairobi.

Wanajeshi wa Kenya, KDF, chini ya muungano wa majeshi ya Afrika kudumisha amani Somalia (AMISOM) wanapambana na wanamgambo wa Al-Shabaab.

Jumamosi wiki jana, Rais Kenyatta akiwa na mkuu wa majeshi Jenerali Mwathethe aliwatembelea KDF nchini Somalia.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako