If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, March 17, 2017

UN: Serikali ya Sudan Kusini ya kulaumiwa kwa baa la njaa; ingali inanunua silaha

Serikali ya Sudan Kusini ndiyo inayobeba lawama kubwa kwa baa la njaa linaloshuhudiwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo iliyoharibiwa na vita huku Rais wa nchi hiyo Salva Kiir akiendelea kutumia mamilioni ya dola zinazotokana na mauzo ya mafuta kuimarisha vikosi vyake vya ulinzi.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la umoja huo na jopo la waangalizi wa vikwazo dhidi ya nchi hiyo.

Waangalizi hao wa UN wamesema, asilimia 97 ya mapato yanayotangazwa rasmi ya serikali ya Sudan Kusini yanatokana na mauzo ya mafuta huku asilimia isiyopungua 50 ya mapato hayo ikitumika kwa masuala ya usalama.

Jopo hilo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limefafanua katika ripoti yake hiyo kuwa mapato yaliyotokana na mauzo ya mafuta yaliyouzwa kuanzia mwishoni mwa mwezi Machi hadi Oktoba 2016 yalikuwa karibu dola milioni 243, lakini licha ya ukubwa wa matatizo ya kisiasa na hali mbaya ya kibinadamu na kiuchumi iliyopo serikali ya Rais Kiir imeendelea kununua silaha kwa ajili ya jeshi lake la Ukombozi la Wananchi wa Sudan (SPLA), vikosi vya huduma za usalama wa taifa, vikosi vingine tanzu pamoja na wanamgambo watiifu kwa serikali hiyo.

Raia wa Sudan Kusini wanaokabiliwa na ukame


Umoja wa Mataifa ulitangaza baadhi ya maeneo ya taifa hilo changa zaidi duniani kuwa yamekumbwa na baa la njaa ambapo watu wapatao milioni tano na nusu, ikiwa ni takriban nusu ya raia wote wa nchi hiyo wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Machafuko na vita vya ndani vilizuka nchini Sudan Kusini Desemba mwaka 2013 baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake, Riek Machar kwamba amehusika na jaribio la kutaka kupindua serikali yake…/

No comments:

Post a Comment

Maoni yako