If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, March 16, 2017

UN yalalamikia utendaji wa serikali ya Burundi kuhusu haki za binadamu

Umoja wa Mataifa umeilalamikia serikali ya Burundi kwa kutoshirikiana na umoja huo katika kuchunguza suala la haki za binadamu nchini humo.

Fatsah Ouguergouz, Mkuu wa Kamati ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu huko Burundi ameeleza kuwa kwa bahati mbaya viongozi wa serikali ya Bujumbura hawakutoa ushirikiano uliohitajika kwa kamati hiyo kwa ajili ya kutambua hali waliyo nayo wahanga wa ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.

Fatsah Ouguergouz ameongeza kuwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vingali vinatia wasiwasai huku Burundi licha ya kuachiwa huru baadhi ya wafungwa wa kisiasa. 

Mkuu wa Kamati ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu nchini Burundi amebainisha kuwa serikali ya Bujumbura imewasilisha taarifa kuhusu uamuzi wake wa kujiondoa katika mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), hata hivyo kamati hiyo inaendelea na shughuli zake na itafuatilia pia masuala ya kisheria yanayohitajika.

Fatsah Ouguergouz, Mkuu wa Kamati ya Uchunguzi ya UN kuhusu Haki za Binadamu huko Burundi


Kwa mujibu wa matamshi ya mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa, serikali ya Burundi tarehe Tatu Januari mwaka huu iliwaachia huru wafungwa kadhaa wa kisiasa, hata hivyo wawakilishi wa taasisi za kijamii, waandishi habari na wanasiasa wa upinzani wa nchi hiyo wanaikimbia nchi kwa kuhofia kutiwa nguvuni. 

Burundi ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa tangu mwezi Aprili mwaka 2015 baada ya Rais Piere Nkurunziza wa nchi hiyo kutangaza azma yake ya kuendelea kusalia madarakani kinyume na katiba.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako