If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, March 16, 2017

UPINZANI KUHUTUBIA TAIFA, ASEMA GLADYS WANGA

Na CHARLES WASONGA

MUUNGANO wa Upinzani (NASA) utatoa hotuba sambamba kwa taifa kujibu ile ya Rais Uhuru Kenyatta, ametangaza Mwakilishi wa Wanawake wa Homa Bay Bi Gladys Wanga.

Bi Gladys Wanga
Mwakilishi wa Wanawake wa Homa Bay Bi Gladys Wanga ahutubia wanahabari Machi 15, 2017 katika majengo ya bunge. Picha/CHARLES WASONGA

Mbunge huyo wa chama cha ODM alipuuzilia hotuba ya Rais kwa Taifa aliyoitoa bungeni Jumatano akisema haikusheheni chochote chenye manufaa kwa Wakenya.

"Rais alitoa wito kwa Wakenya kuipigia kura serikali ya Jubilee kwa mara nyingine. Kwa nini Wakenya wachague serikali iliyojaa ufisadi na inayoongozwa na viongozi wenye hasira? Tutaanika maovu ya serikali hii kwenye hotuba kwa Taifa ambayo Nasa itatoa hivi karibuni," Bi Wanga akasema katika majengo ya bunge baada ya kukamilika kwa hotuba ya rais Kenyatta.

Alipinga kauli ya Rais kwamba serikali ya Jubilee ndiyo ilijenga daraja linalounganisha kisiwa cha Rusinga katika Ziwa Victoria na ufuo wa Mbita akisema mradi huo ulitekelezwa na utawala uliopita chini ya rais mstaafu Mwai Kibaki na kinara mwenza wa Nasa, Raila Odinga.


"Rais alihadaa Wakenya, katika hotuba yake, kwa kudai kuwa utawala wake ndio ulijenga daraja la linalounganisha kisiwa cha Rusinga na eneo la Mbita. Huu ni mradi wa serikali ya nusu mkate," akasema Wanga anayewakilisha eneo hilo.

Mishahara

Kuhusu wazo la kupunguzwa kwa mishahara ya maafisa wa serikali wanaopokea mishahara ya juu mbunge huyo alilipinga akisema halina mantiki yoyote.

"Kabla ya kupunguza mishahara ya wabunge na maafisa wengine wa umma serikali ya Jubilee inapasa kuwajibikia Sh300 bilioni ambazo hupotea kila mwaka kupitia kashfa za ufisadi," Bi Wanga akasema.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako