If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, March 24, 2017

UTAWALA WA MAGUFULI WAGEUKA KUWA HASI?

Na MWANGI MUIRURI

Utawala wa rais John Pombe Magufuli wa Tanzania ambao umedumu tangu Oktoba 2015 umejipata katika darubini ya uchanganuzi ikiwa ni utawala wa haki au hasi.

Rais John Magufuli akitoa hotuba
Rais John Magufuli akihutubu awali. Picha/AFP

UTAWALA wa rais John Pombe Magufuli wa Tanzania ambao umedumu tangu Oktoba 2015 umejipata katika darubini ya uchanganuzi ikiwa ni utawala wa haki au hasi.

Visa vya rais huyo ambaye alipotawazwa mashindi na siku chache baadaye akawa amevishwa jina tingatinga kufuatia ubabe wake wa kujisukuma kiume dhidi ya vizuizi vya utawala mbaya kulingana na maoni yake sasa vimegeuka kuwa vya kutiliwa shaka.

Kwa mujibu wa mchanganuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini Gasper Odhiambo 'mgema akisifiwa, tembo hulitia maji'.

"Kuna visa ambapo Magufuli amejidhihirisha kuwa na utawala wa maono kama vile vya kushiriki usafishaji wa mazingira na kukataa madaraja yapewe jina lake lakini kwa vingine yeye ni mweledi wa kutofuata sheria,” asema Odhiambo.

Anasema kuwa visa vya rais Magufuli kuvamia idara za serikali na kutangaza kuwa amemfuta huyu na yule kazi bila hata ya kuwapa nafasi ya kujitetea ni mfano bora wa rais asiyejali kuwapo kwa sheria za kulinda haki za binadamu—wawe wazuri au wabaya.


Anasema kuwa rais Magufuli pia amedhihirisha kuwa angetaka Tanzania ibakie kama kisiwa cha uongozi wa kipekee usioshirikiana na mataifa mengine hasa yaliyo katika jumuia ya Afrika mashariki.

“Ni rais ambaye kuzielewa sera zake za kigeni ni vigumu. Afisi ya urais iko ndani ya kichwa chake na yeye ndani ya afisi hiyo ndiye kinara na hakuna mwingine juu yake au kando yake katika kutekeleza maamuzi. Ni uongozi ambao polepole unajipa taswira ya udikteta,” asema.

Akiwa mamlakani kwa ushindi wa asilimia 58.46 ya kura, Magufuli anafaa kuelewa kuwa ule ubabe wa serikali kuwa na uthabiti wa ukiritimba umeisha katika taifa la Tanzania na kwa sasa kuna sauti kubwa inayokaribia umaarufu wa serikali ya upinzani.

Peter Kagwanja ambaye ni msomi na mchanganuzi wa kisiasa anasema kuwa

Magufuli ako na ile kasumba kwamba bado anaishi katika ile enzi ya kutokuwapo na ushindani wa kisiasa Tanzania ili hali atakuwa anajikosea akielewa jinsi alivyotolewa kijasho katika uchaguzi uliompisha uongozini.

“Ni rais aliyeingia mamlakani na akapata umaarufu wa kimrengo katika jumuiya ya wale waliobobea siasa za ukiritimba… Wale ambao bado hawajang’amua ukweli wa mambo kuwa demokrasia imekua kwa kasi nchini Tanzania… Umaarufu huo wa kutwikwa majina ya mchapa kazi na kushangilia hata anapokosea unamwelekeza kuzidisha kujikwaa kwake kiutawala,” asema.

Hata hivyo, anasema kuwa huenda upinzani unaopata umaarufu kwa kasi nchini Tanzania ndio unachangia kuzorota kwa kukubalika kwa Magufuli kama rais aliyefaa na anayefaa Tanzania kwa sasa na siku zijazo pia.

“Unajua siasa huwa na ujeuri mwingi. Huenda labda kuna mrengo wa upinzani ambao unafadhili njama za kumwangazia Magufuli kama anayepotokwa na uthabiti wa kimaamuzi. Jinsi muda unavyozidi kuyoyoma Tanzania ikieleka kwa uchaguzi mwingine ndivyo jinsi upinzani utajaribu kumpokonya umaarufu wake na aishie kuwa na magurudumu yaliyotoboka kisiasa,” asema.

Anasema kuwa kisa cha hivi karibuni ambacho kimewasha moto wa udhalimu wa serikali ya Magufuli kinahusu kuvamiwa kwa kituo kimoja cha Televisheni nchini humo na wandani wa rais wakiwa wamejihami na ambapo walitekeleza yote ambayo kisheria ni ujambazi.

Katika kisa hicho cha uvamizi sawa na kile kilichotekelezewa kampuni ya Standard Group nchini Kenya 2006 kiliongozwa na mshirikishi wa utawala wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiandamana na wenzake waliojihami.

Kampuni hiyo ya utangazaji ya kibinafsi kwa jina Clouds FM Media Group kilijipata pabaya na ukonde wa kimawazo wa Makonda kwa msingi kuwa kilikataa kupeperusha habari za mkanda wa video kuhusu utundu wa kingono dhidi ya pasta mmoja aliye katika mgogoro na huyo Makonda.

Habari zilikuwa pasta huyo ako na motto haramu nje ya ndoa, mlalamishi akiwa ni mwanamke mzazi wa mwana huyo.

Waziri wa mawasiliano wa Tanzania aliyevuliwa cheo hicho Alhamisi, Nape Nnauye, akiwa katika mkondo wake wa kusimama na haki kwa mujibu wa sheria na miongozo ya taaluma ya uanahabari akashutumu uvamizi huo huku akiamrisha suala hilo lipigwe msasa.

Aliteta kuwa “uvamizi kama huo tumeuzoea katika ujambazi wa kupindua serikali ambapo 'wahalifu' huvamia studio za taaluma ya uanahabari ili kutangaza kuwa wao (wahalifu) ndiyo wako usukani wa serikali.”

Nembo mbaya

Huku akiamini kuwa Magufuli alikuwa katika mstari wa kutii sheria na utawala bora, Nnauye alisisitiza kuwa uvamizi huo uliangazia serikali kwa nembo mbaya “na kwa uhakika nitashauriana na wakubwa wangu serikalini ili wamuadhibu Makonda.”

Ikawa ni hali ya kustusha Magufuli kumtimua Nnauye serikalini na hatimaye akamtetea makonde kwa njia zote za uwezo wake wa ufasaha wa lugha.

“Mimi ndio Rais, hakuna wa kunielekza nifanye nini kuhusu lipi. Mimi pekee ndiye wa kuamua nani awe wapi na wewe Makonda fanya kazi yako na usijihusishe na taharuki kuhusu lolote,” akasema Magufuli.

Gasper Odhiambo anasema kuwa “hayo ni matamshi ya dikteta asiyesemezeka wala haambiliki na ndugu zetu wa Tanzania wako na vita mbele yao ya kujikomboa kutokana na kujiunda kwa wingu la utawala wa kukandamiza kila aina ya haki maishani mwao.”

Anasema kuwa urafiki wake wa karibu na wanasiasa wabishi wengi ambao wametuhumiwa na siasa za ujambazi na umwagikaji wa damu “ni dhihirisho tosha kuwa Watanzania walihadaiwa kumkumbatia Magufuli kama rais na njia ya kipekee ya kumthibiti ni kuamsha upinzani unaokisiwa kuwa na ufuasi wa asilimia 45.”

Kufikia sasa, Deodatus Balile, ambaye ni mwenyekiti wa jopo la kuchunguza uvamizi huo wa kituo cha Televisheni ashatoa ripoti kuwa Makonde alikuwa amewatishia maisha wanahabari wa kampuni hiyo iwapo wangekaidi kupeperusha habari hizo za pasta na ujeuri wake wa kingono.

Katika hotuba yake ya kuiga kazi yake ya uwaziri, Nnauye alisisitizia Watanzania kuwa “msijali na hatua yangu kutimuliwa kazini bali mnafaa mjitahadharishe na kwenye Tanzania inaelekezwa kiutawala.”

Odhiambo anasema hapo ndipo jibu la sura kamili ya Magufuli inaanikwa “kwa kuwa kwenye anaelekeza Tanzania sio kwa kujivunia kama sisi sote Waafrika bali ni kufuata zile nyayo tu za madikteta wengine wa Afrika.”

Anasema kuwa nia kuu ya magufuli ni ya kujijenga kama mhasi sugu asiyechezewa huku akijiandaa kuendeleza mbele utawala wake kimabavu akilenga kujithibiti mamlakani ili kuogofya wakereketwa ambao wanaweza wakajiunga na upinzani wa kumtimua mamlakani.

Chanzo: swahilihub.com

1 comment:

  1. labda pengine kwakuwa uko mbali na tanzania au kama unavyosema ameandika odhiambo hata sijui kama ni mtanzania au mkenya u know better..sasa sisi tuliopo huku nyumbani ambao tunayaona na kushuhudia nachoweza kwambia ni kwamba ni kundi tu la watu wachache ambao wanania ya kuichafua serikari na kuvuruga amani ya nchi kupitia mitandao ya jamii,waandishi wa habari kama wewe na saa nyingine hata viongozi wa serikari pia nao wamekuwa wakitumiwa na ndio maana unaona kila inapogundurika inafanyika reform na maisha yanaendelea kwaiyo nikutoe tu wasiwasi sisi huku tanzania tuko zaidi ya vizuri na mambo ni tambalale tuna heshimiana na amani ni tele labda wewe na hao masnitch wenzio sasa ndio mje kutuvuruga..goodday

    ReplyDelete

Maoni yako