If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, March 21, 2017

Uturuki: Kuonyeshwa picha za wapinzani wetu Ujerumani, ni uadui dhidi yetu

Mvutano katika uhusiano kati ya Uturuki na Ujerumani umechukua sura mpya baada ya viongozi wa Ankara kulalamikia hatua ya kupendelewa wapinzani wake nchini humo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki sambamba na kulaani hatua hiyo ya Ujerumani, imesema kuwa kitendo cha kuonekana picha za viongozi wa chama cha wafanyakazi wa Kikurdi (PKK) na kutolewa nara dhidi ya serikali ya Uturuki katika maandamano yaliyofanyika hivi karibuni nchini Ujerumani, ni suala lisilokubalika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki pia imesisitiza kuwa, Ujerumani imekuwa ikifuata mkondo wa uhasama dhidi yake kiasi cha kutowaruhusu mawaziri na wabunge wa nchi hiyo kukutana na raia wa Uturuki waishio nchini humo. 

Hivi karibuni, mkuu wa idara ya intelejensia ya Ujerumani, Bruno Kahl alinukuliwa akitilia shaka kampeni ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali ya Uturuki dhidi ya kundi la harakati ya Jama'at G├╝len ambaye pia ni mpinzani wa serikali ya Ankara kuwa ni kundi la kufurutu ada au la kigaidi.

Kiongozi wa wapinzani wa serikali PKK


Kwa mujibu wa afisa huyo wa intelejensia wa Ujerumani, viongozi wa Uturuki wamekuwa wakifanya juhudi kubwa katika ngazi tofauti kwa ajili ya kuwashawishi walimwengu kuitambua harakati hiyo kuwa ya kigaidi. 

Hivi karibuni serikali za Ujerumani na Uholanzi ziliwazuia viongozi wa serikali ya Ankara kuendesha kampeni za uchaguzi wa kura ya maoni katika nchi hizo, sambamba na kuwaruhusu wanachama wa chama cha wafanyakazi wa Kikurdi (PKK), kuweza kuhutubia Ulaya, suala ambalo limeichukiza mno Uturuki..

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako