If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, March 20, 2017

Wanafunzi zaidi ya 20 wafa maji wakiogelea nchini Ghana

Kwa akali wanafunzi 20 wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na miti walipokuwa wakiogelea katika chemchemu ya maji nchini Ghana.

Prince Billy Anaglate, Msemaji wa Idara ya Zimamoto nchini humo amesema kuwa, mkasa huo ulifanyika jana alasiri wakati kundi la wanafunzi wa shule ya sekondari walipokuwa wakiogelea katika chemchemu ya maji ya Kintampo, katika eneo la Brong-Ahafo, lenye vivutio vingi vya utalii.

Ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, upepo mkali ulijiri na kung'oa miti iliyowaangukia wanafunzi hao na kuwaua walipokuwa wakiogelea katika chemchemu hiyo.

Chemchemu ya Kintampo nchini Ghana

Afisa huyo wa Idara ya Zimamoto nchini Ghana ameongeza kuwa, wanafunzi 11 walifariki dunia papo hapo, na wengine 9 walipoteza maisha walipokuwa wakitibiwa baada ya kuokolewa.

Catherine Abelema Afeku, Waziri wa Utalii wa Ghana ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa ajali hiyo na kuwatakia afueni ya haraka waliojeruhiwa katika tukio hilo la jana.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako