If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, March 10, 2017

WANAWAKE WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUTAFUTA UONGOZI

Na LAWRENCE ONGARO

WANAWAKE kote nchini wamehimizwa kujitokeza ili kugombea viti vya uongozi kwa ukakamavu.
Mwaniaji wa kiti cha mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kiambu, Bi Lydia Njeri, amewataka wanawake wasikae kitako huku wakingojea kuteuliwa bungeni ama katika nyadhifa zingine tofauti.

Lydia Njeri
Mwaniaji wa kiti cha mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kiambu, Bi Lydia Njeri. Picha/LAWRENCE ONGARO

"Sioni ni kwa nini wanawake wanajiona kama wanyonge huku tumaini lao likisalia la kupata uteuzi," alisema Bi Njeri.

Alisema wakati huu mambo yanastahili kubadilika kwa wanawake kuwa mstari wa mbele kutete haki yao katika uongozi wa nchi.

Kila mwanamke anayejiona kuwa anatosha kuwasilisha ajenda yake kwa wananchi afanye hivyo bila kuchelewa kwa vile wakati huu ni wao wa kujitambulisha,'' alisema Bi Njeri.

Alisema ili kiongozi kujipata kileleni, ni sharti ajizatiti na kutafuta kile anachokiihitaji.

Aliyasema hayo mnamo Jumatano mjini Ruiru alipohutubia waandishi wa habari akiwapa mwongozo wake wa kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 8, 2017.

"Wakati wa wanawake kungojea kupewa uongozi kwa urahisi umepitwa na wakati na kwa hivyo kila mwanamke anayetamani uongozi lazima ajitokeze hadharani kwa wananchi ili wamkague na kumtathmini kabla ya kupewa nafasi ya kuongoza,'' alisema Bi Njeri.


Alisema wanawake ni watu wenye vipaji vingi kwa vile ni wazi ya kwamba mwanamke ndiye ngunzo ya kuendesha familia na ni wao huwa na mzigo mwingi.

Alibashiri ya kwamba ifikapo mwaka wa 2022 pengine mwanamke atateuliwa kuwa mgombea mwenza kwa maana ya kuwa naibu wa rais wa kwanza nchini.

Alitoa wito kwa wanawake kuwapigania wanawake wenzao ili kuafikia malengo yao ya kupata uongozi.

"Wanawake wanastahili kuwaunga mkono wenzao ili nao waweze kufika kileleni, ambapo bila kufanya hivyo bado tutakuwa tukijilaumu sisi wenyewe," alisema Bi Njeri na kuongeza mwanamke anastahili kumpenda mwanamke mwenzake ili kufanya mabadiliko hayo.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako