If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, March 3, 2017

Watu wa Canada wataka bidhaa za Israel zisusiwe

Watu wa Canada wametaka bidhaa zinazotegenezwa Israel zisusiwe nchini humo kama njia ya kutetea haki za taifa la Palestina.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika Lisilo la Kiserikali ya "Canada kwa ajili ya Uadilifu na Amani Mashariki ya Kati" uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa, raia wa Canada mbali na kuafiki azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo limelaani ujenzi wa vitongozi vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina, pia wametaka utawala wa Israel uwekewe vikwazo .

Aghalabu ya walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni wamelaani vikali namna utawala wa Kizayuni wa Israel unavyokiuka sheria za kimataifa na kwa msingi huo wamesema ni jambo la kimantiki kususia bidhaa za Israel.

Maandamano ya kuunga mkono ususiwaji Israel

Harakati ya kimataifa ya kuiwekea vikwazo Israel inayojulikana kwa jina la Boycott, Divestment and Sanctions against Israel BDS, inaendelea kuimarika kimataifa kutokana na uungaji mkono mkubwa inaopata kutoka kwa jumuiya za viwanda, makundi ya kidini, mashirika yasiyo ya serikali na serikali zinazoungwa mkono na wananchi. 

Ni wazi kuwa vikwazo ambavyo vimekuwa vikitekelezwa dhidi ya utawala wa Kizayuni vimekuwa na matokeo makubwa hasi ya kisiasa, kidiplomasia, kiutamaduni na kiuchumi kwa utawala huo. Hivi sasa utawala wa Kizayuni wa Israel umeingiwa na wasiwasi mkubwa kutokana na mafanikio ya harakati hiyo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako