If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, March 20, 2017

Waziri Mkuu wa Somalia: Saudia, mhusika wa mauaji ya wakimbizi wa Kisomali

Serikali ya Somalia imesema kuwa utawala wa Saudi Arabia ndio uliohusika na mauaji ya wakimbizi wa nchi hiyo katika maji ya Yemen.

Waziri Mkuu wa Somalia, Hassan Ali Khayre ametoa taarifa akilaani mauaji ya wakimbizi wa Kisomali yaliyofanywa na helikopta ya jeshi la Saudi Arabia karibu na pwani ya Yemen na kusema kuwa, wahanga hao wameuawa bila ya hatia yoyote na wengi wao walikuwa wanawake na watoto wadogo.

Waziri Mkuu wa Somalia ameitaka serikali ya Saudia pia kufanya uchunguzi kuhusu mauaji hayo.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia, Abdisalam Omer amesema yaliyowakuta wakimbizi wasio na hatia yoyote wa Somalia ni maafa ya kushtua na kutisha na kusisitiza kuwa Saudi Arabia imehusika na jinai hiyo.

Maiti za Wasomalia waliouawa na Saudi Arabia

Ripoti zinasema kuwa, wakimbizi hao wa Kisomalia waliokuwa katika boti wakielekea Yemen waliwasha tochi ili kuwaonesha askari wa Saudia kuwa si wanamgambo lakini helikopta ya jeshi la Saudia na meli moja ya kivita hazikujali alama hizo na badala yake ziliwamiminia risasi wakimbizi hao na kuwaua kikatili.


Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa, wakimbizi wasiopungua 44 wa Somalia wameuawa katika shambulizi hilo na wengine 80 wamejeruhiwa.

Shirika la Kimataifa la Wahajiri (IOM) na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) yalilaani vikali mauaji hayo ya kinyama dhidi ya raia ambao hakuwa na silaha.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako