If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, March 11, 2017

ZADIA NA PURE ULTRASOUND KUSAIDIA VIFAA VYA ULTRASOUND ZANZIBAR

ULTRASOUND ZANZIBAR

Hospitali za Zanzibar zinatarajiwa kufaidika na vifaa vya kisasa vya Ultrasound kwa ajili ya kuboresha sekta ya Afya visiwani humo.


Jumla ya Hospitali tatu za Pemba zinatazamiwa kufaidika na vifaa hivyo baadda ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mafunzo ya kitaalamu juu ya matumizi ya vifaa hivyo yaliyoanza Jumatatu wiki hii.

Mafunzo hayo yanayoendelea katika Ukumbi wa Maabara Kuu ya Afya iliyoko Wawi, Wilaya ya Chake Chake kisiwani humo, yanaendeshwa na wataalamu wa fani hiyo kutoka Shirika la Pure Ultrasound la nchini Marekani.

Mradi huu ni matunda ya juhudi za Jumuiya ya Wazanzibari waishio Nchini Marekani (ZADIA) za kusaidia harakati za maendeleo visiwani Zanzibar katika nyanja tofauti.

Katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo iliyosomwa kwa niaba yake na Mwakilishi wa ZADIA Bwana Dhamir Ramadhan, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Bwana Omar H. Ali alisema kuwa jumuiya yake inaelewa umuhimu wa afya bora kwa ajili ya mendeleo.

"ZADIA inaelewa vyema umuhimu wa afya kwa mwanadamau, na kwamba bila ya kuwa na jamii iliyo na afya njema, basi hakutokuwa na uwezo wa kutekeleza shughuli za maendeleo". Alisema Bwana Ali, na kuoungeza: "Aidha, inaelewa fika kuwa Maradhi ni mmoja kati ya maadui wakubwa wa maendeleo ya mwanadamu, akishirikiana na wenzake Ujinga na Umaskini. "

Mafunzo hayo yanawashirikisha zaidi ya Madaktari 15 kutoka Hospitali za Wilaya za Chake-Chake, Wete na Micheweni, na yanatazamiwa kudumu kwa muda usiopungua miezi 6.

Bwana Ali aliwahimiza Madaktari wanaoshiriki katka mafunzo hayo, kujifunga vibwebwe katika kuhakikisha wanapata ujuzi wa kutosha baada ya mafunzo yao kumalizika, na kuutumia ujuzi huo kwa maslahi ya taifa.


"Fungeni vibwebwe vyenu na mikuti yenu ili muchukue kila neno na kitendo mnachooneshwa. Hakikisheni utaalam wote unaohitajika ikimalizika kazi ya kujifunza mumeuchukua na muwe tayari kuwatumikia ndugu zetu na pia kuwafundisha wengine kwa niaba yetu". Alisisitiza Bwana Ali.
Aliendelea kusema kuwa mara baada ya kukamilika kwa mafunzo ya kisiwani Pemba, ZADIA itaendelea na juhudi zake ili kuanza awamu ya pili ya mradi huo kisiwani Unguja.

"Mara tu baada ya kukamilika mafunzo kwa wataalamu wetu wa Hospitali za Pemba, ZADIA itaongeza bidii ili zoezi hili liendelee katika Hospitali za Unguja", alisema Bwana Ali na kuongeza "Tunatarajia wadau wetu PURE ULTRASOUND watakuwa nasi kwa kazi hii".

Kwa upande wake Naibu Asifa Mdhamini wa Wizara ya Afya Pemba Bwana Ayoub Mohammed Shoka, aliwataka washiriki katika mazunzo hayo kuchukua juhudi za dhati katika kuhakikisha kuwa wanafanikiwa kupata ujuzi uliokusudiwa katika mafunzo hayo, na kutokuwa na wivu wa kuwafundisha wengine.
Aidha, alitoa shukrani zake kwa ZADIA, Shirika la Pure Ultrasound na Shrikila la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa juhudi zao za kufanikisha mradi huo.

Itafaa kudokeza kuwa Mradi huu Uliotokana na juhudi za ZADIA, unaendeshwa na Shirika la Pure Ultrasound la Nchini Marekani ambalo limetoa wataalamu wanaoendesha mafunzo hayo kwa ushirikiano na Wizara ya Afya Zanzibar, pamoja na UNESCO ambayo imetoa Mashine tatu kwa ajili ya mafunzo hayo.

Mradi huu utakapokamilika, utasaidia sana katika kuwawezesha madaktari wa Zanzibar kitaaluma, khusuan katika fani za kinamama waja wazito na wazazi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako