If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, April 26, 2017

GAVANA RASANGA ASHINDA TIKETI YA ODM SIAYA

Na CHARLES WASONGA

SHANGWE, vifijo na nderemo zilitanda mjini Siaya Jumatano asubuhi baada ya Gavana wa kaunti hiyo Bw Cornel Rasanga Amoth kutangazwa mshindi wa katika kinyang'nyiro cha kuwania tiketi ya kuwania kiti hicho kwa tiketi ya ODM.

Cornel Rasanga
Gavana wa Siaya Cornel Rasanga. Picha/MAKTABA

Rasanga alizoa jumla ya kura 143,446 na kumshinda mpinzani wake Mbunge wa Rarieda Nicholas Gumbo aliyepata kura 87,467.

Hata hivyo, Bw Gumbo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Uhasibu (PAC) alipinga matokeo hayo akidai kulikuwa na udanganyifu mkubwa katika shughuli hiyo.

"Msimamizi wa uchaguzi aliyetangaza matokeo hayo ni mwanasarakasi tu. Hakutangaza matokeo halisi. Huu ni ukora ambao ulianza katika vituo vya kupigia kura," amesema Bw Gumbo ambaye alisema atashauriana na wafuasi wake kusaka mkondo mpya wa kisiasa.

Wizi

Mbunge wa Bondo Bw Gedion Ochanda pia alipinga matokeo hayo akisema Gavana Rasanga alitumia wafanyakazi wa kaunti kuiba kura.
Duru zimearifu Swahilihub kwamba Bw Gumbo anapanga kugombea kiti hicho kama mgombeaji huru.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako