If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, April 15, 2017

ISAAC RUTO: INFOTRAK IKOME KUENEZA PROPAGANDA

Na RUTH MBULA

GAVANA wa Bomet Bw Isaac Ruto amepuuzilia mbali matokeo ya kura ya maoni iliyofanywa na shirika la utafiti la Infotrak na kuonyesha atakumbwa na ushindani mkali kutoka kwa Naibu Spika wa bunge la taifa, Dkt Joyce Laboso.

Gavana wa Bomet Isaac Ruto
Kiongozi wa Chama cha Mashinani (CCM) aliye pia gavana wa Bomet Isaac Ruto akihutubu awali. Picha/TONNY OMONDI

Matokeo ya utafiti huo yalionyesha Bw Ruto wa Chama Cha Mashinani akiongoza kwa asilimia 38.9 ya kura, huku Dkt Laboso anayepanga kugombea tikiti ya Jubilee akimfuata kwa asilimia 37.7.

Kwenye mahojiano na Taifa Leo Jumamosi, Bw Ruto alisema utafiti huo ni propaganda tupu zilizonuiwa kuhadaa wakazi wa Bomet kuunga mkono Jubilee katika uchaguzi wa Agosti 8.

“Kura hiyo ya maoni haipotoshi tu, bali pia ililenga kupendelea Jubilee na kutoa ishara kwamba mgombeaji wao anaungwa mkono na idadi kubwa zaidi ya wapigakura wa Bomet,” akasema Bw Ruto.

Dkt Laboso atapigania tikiti ya Jubilee na Dkt Julius Kones kwenye kura ya mchujo itakayofanyika Aprili 21.


Katika utafiti huo, ilibainika kuwa Jubilee ni maarufu zaidi ikiwa na ufuasi wa asilimia 73, huku CCM ikiwa na asilimia 12 pekee.

Hata hivyo, Bw Ruto alisema chama chake kimezidi kupata umaarufu katika eneo la South Rift na Jubilee imeanza kubabaika baada ya umaarufu wake kuanza kufifia.

“(Dkt Laboso) atapata wapi hata asilimia 40 za kura katika kaunti hii ilhali wakazi ni wafuasi sugu wa CCM katika ushindani wa ugavana, useneta, ubunge na udiwani?” akauliza.

Aliongeza: “Ninatoa wito kwa wafuasi wa CCM ya Bomet wapuuze kura hiyo ya maoni.”

Chanzo: swahilihub.com/

No comments:

Post a Comment

Maoni yako