If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Sunday, April 16, 2017

JUBILEE YAPIGA MARUFUKU KADI ZA UANACHAMA KWA MCHUJO

Na CHARLES WASONGA

CHAMA cha Jubilee (JP) kimepiga marufuku matumizi ya kadi maalum za uanachama katika chaguzi za mchujo zitakazofanyika Ijumaa ijayo, Aprili 21 kati kaunti 33.

Jubilee Party
Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kwenye hafla ya uzinduzi wa kadi ya kielektroniki ya uanachama wa Jubilee Party uwanjani Safaricom-Kasarani Januari 13, 2017. Picha/SWAHILIHUB

Katibu Mkuu Bw Raphale Tuju Ijumaa alisema chama hicho kitatumia sajili ya wanachama wake kuwatambua wapigakura halisi watakaoruhusiwa kushiriki zoezi hilo. Aliongeza kuwa kadi hizo zitatumika tu kama stakabadhi za ziada za kuwatambua wanawachama wa Jubilee.

"Tumebaini kuwa baadhi ya wanachama, haswa wawaniaji viti walinunua kadi hizo kwa wingi na kusambazia wafuasi wao kwa matumaini kuwa wangezitumia kuwapigia kura wakati wa mchujo.

Ole wenu mlioendesha ukora huo kwa sasa kadi hizo hazitahitajika siku ya mchujo. Tutatumia sajili ya wanachama," Bw Tuju akawaambia wanahabari katika Chuo Kikuu cha Multimedia ambako maafisa wa kusimamia mchujo walikuwa wakipokea mafunzo.

Alikuwa ameandamana na Mwenyekiti wa Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi (NEB) ya chama hicho Bw Andrew Musangi pamoja na wanachama wengine wa bodi hiyo.

Akiunga mkono kauli ya Bw Tuju, Bw Musangi alisema kuwa bodi yake iligundua kuwa wafuasi wa JP kutoka baadhi ya maeneo nchi hawakuwa wamepata kadi hizo za uanachama.


"Kwa sababu sio wote walipata nafasi ya kununua kazi hizo, tumeamua kwamba sajili ya wanachama wa Jubilee iliyotolewa na msajili wa vyama vya kisiasa ndio itumiwe katika mchujo," akasema.

Alisema kulingana na sajili hiyo chama hicho kina zaidi ya wafuasi milioni nane, na kuifanya kuwa chama chenye wafuasi wengi zaidi nchini.

Bw Musangi alisema kuwa karatasi za kupigia kura zitakazotumika katika mchujo zimechapishwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambapo haziwe kughushiwa.

"Karatasi hizo zina alama za usalama na ni za rangi tofauti kuambatana na wadhifa unaogombaniwa. Kwa mfano, rangi ya karatasi za kura za udiwani ni tofauti za zile za ugavana, useneta au ubunge," akaeleza mwenyekiti huyo ambaye ni mtaalamu wa masuala ya sheria.

Bw Musangi alisema masunduku ya kupigia kura yametengenezwa kwa njia ya kisasa hivi kwamba hayawezi kufunuliwa kwa njia rahisi kuendeleza njama ya wizi wa kura.

"Sanduku hizo zitafunguliwa katika vituo vya kupigia kura mbele ya maajenti wa wawaniaji," akasema.

Bw Tuju alisema kuwa chama hicho kitahakikisha kuwa zoezi hilo limeendeshwa kwa njia huru, haki na uwazi ili kuhakikisha kuwa watakwa ya wananchi yanaheshimiwa.

"Hii ndio maana tumewaidhinisha waangalizi kutoka mashirika ya kimataifa kutathmini jinsi tutakavyoendesha shughuli hiyo katika vituo mbalimbali kote nchini. Baadhi ya waangalizi hao ni: Ubalozi wa Amerika, Ubalozi wa Uingereza, Umoja wa Ulaya (EU) na mashirika mengine ya kigeni," akasema Bw Tuju.

Katibu huyo mkuu aliongeza kuwa chama hicho kimeamua kuwabadilisha maafisa wa kusimamia uchaguzi ili kuzuia visa vya upendeleo.
"Kwa mfano, maafisa wanaopokea mafunzo hapa (Chuo Kikuu cha Multimedia) hawajui mahala ambapo watatumwa kusimamia mchujo.

Tutafanya mabadiliko hayo dakika za mwisho; hivi kwamba maafisa kuto Pokot Magharibi wanaweza kutumwa kuendeshwa mchujo katika kaunti ya Murang'a," akasema Bw Tuju./

No comments:

Post a Comment

Maoni yako