If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, April 12, 2017

KAMATI YA NASA YAKANA RIPOTI ZA 'RAILA TOSHA'

Na VALENTINE OBARA

KAMATI ya Kitaifa ya Uratibu (NCC) katika Muungano wa NASA Jumatano ilijitenga na ripoti iliyoonyesha Kiongozi wa Chama cha ODM Bw Raila Odinga ndiye atakayepeperusha bendera ya muungano huo kwenye uchaguzi wa urais.

Kamati ya Kitaifa ya Uratibu
Kutoka kushoto: Wanachama wa Kamati ya Kitaifa ya Uratibu (NCC) ya Muungano wa NASA Mbunge wa Tongaren Eseli Simiyu (Ford Kenya), Seneta wa Siaya Bw James Orengo (ODM), , Seneta wa Machakos Johnstone Muthama na Mbunge wa Nambale Sakwa Bunyasi (ANC) walipohutubia wanahabari Aprili 12, 2017. Picha/ VALENTINE OBARA

Kamati hiyo inayojumuisha Seneta wa Siaya Bw James Orengo (ODM), Mbunge wa Tongaren Eseli Simiyu (Ford Kenya), Seneta wa Machakos Johnstone Muthama na Mbunge wa Nambale Sakwa Bunyasi (ANC) ilisema wanachama wao waliozungumzia ripoti hiyo hawana mamlaka kutoa taarifa rasmi kwa niaba ya NASA.

Mnamo Jumanne, Kaimu Katibu Mkuu wa ODM Dkt Agnes Zani alitoa taarifa kwa vyumba vya habari kusema ripoti hiyo iliyoonyesha Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka atakuwa mgombea mwenza wa Bw Odinga, ilikuwa sahihi na ilifahamika na wadau wote katika NASA.

“Sisi ndio wenye mamlaka katika NASA...mbona msikilize watu wengine ambao hawana mamlaka?” akasema Bw Orengo katika kikao cha wanahabari afisini mwake Nairobi.


Bw Orengo alisema kuna ripoti moja pekee ambayo kamati hiyo imekabidhi kwa vinara wa muungano huo kufikia sasa, na ni ripoti ambayo haijakamilika, na wanatayarisha ripoti nyingine itakayojadiliwa na vinara wao watakapokutana faraghani hivi karibuni.

Walipuuzilia mbali dhana kuwa kuna mgawanyiko miongoni mwa wafuasi wao na kusema yale yanayoshuhudiwa ni utekelezaji wa haki ya kidemokrasia ya wanachama kujieleza.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako